NA VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mwenyekiti wa Umoja wa wanawake (UWT) Wilaya ya ya Kibaha mjini Elina Mgonja amewataka wanawake kuachana na tabia ya kukaa vijiweni na badala yake wanapaswa kubadilika na kujiunga na vikundi vya ujasiriamali ili kuweza kujikwamua kiuchumi.
Elina ametoa kauli hiyo wakati akizungumza na wanawake wa UWT Kata ya picha ya ndege wakati wa mwendelezo wa ziara yake ya kikazi ya kuweza kujionea uhai wa chama pamoja na kuwahimiza kujitokeza kuchukua fomu kwa ajili ya kugombea nafasi za uongozi.
Mwenyekiti huyo alibainisha kwamba wanawake wanatakiwa kujituma kwa bidii katika kufanya kazi mbali mbali ambazo zitaweza kuwasaidia kuondokana na wimbi la umasikini na kuondokana na kuwa tegemezi.
"Wanawake mnapaswa kuwa wajasiri katika kushiriki katika kazi mbali mbali ikiwa ni pamoja na kujiunga katika vikundi mbali mbali vya ujasiriamali ili kuweza kujikwamua kiuchumi na kuondokana na kuwa tegemezi,"alisema Mgonga.
Pia aliwataka wanawake kuhakikisha wanatengeneza mahusiano mazuri na viongozi mbali mbali wa chama cha mapinduzi na viongozi wa serikali katika shughuli mbali mbali za utekelezaji wa maendeleo.
Aidha aliwahimiza wanawake kuwa mstari wa mbele katika kumuunga mkono Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan katika kutekeleza majukumu yake ya kila siku.
Kadhalika Elina alisema kwamba wanawaje wa UWT wanatakiwa kuwa na umoja na mshikamano hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa lengo ikiwa ni kushinda katika mitaa yote.
Kwa upande wake Katibu wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini Cesilia Ndalu amesema wanawake wanatakiwa kuwa na ushirikiano na upendo kwa lengo la kuweza kukijenga na kukiimarisha chama cha mapinduzi.
Ziara ya Mwenyekiti wa UWT Wilaya ya Kibaha mjini ina lengo la kutembelea wanawawake wa UWT katika kata mbali mbali ili kuona uhai wa chama sambamba na kuhimiza wanawake kujitokeza kuchukua fomu za kuwania uongozi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.