MAKONDA AANDIKA HISTORIA MPYA UENEZICCM
- Ni kuwa Mwenezi aliyehudumu muda mfupi kuliko wenezi wote tangu CCM iundwe - licha ya mbwembwe na sarakasi zake amedumu kwa miezi mitano na wiki moja tu kitini, muda mchache kuliko Shaka aliyekaa miaka miwili kasoro na Sofia Mjema aliyekaa miezi kumi kwa awamu ya sita - kuondolewa kwake kwaibua mijadala wengi wakimpongeza Rais Dkt Samia kuendelea kuisuka vyema sektetarieti ya CCM na kuimarisha Serikali - wengine wasema hawakutaraji kama angefika hata miezi miwili kwenye kiti hicho kutokana na kauli na matendo yake - Kibarua kigumu kwa mrithi wake Akitarajiwa kutekeleza hasa shughuli za kikatiba za mwenezi badala ya kujikita kwenye maigizo mfano wa sinema za kihindi kama kwa mtangulizi wake "Idara ya Itikadi na Uenezi ni kitengo nyeti na muhimu ndani ya CCM...Miongoni mwa majukumu ya idara hiyo ni kushughulikia na kueneza masuala ya itikadi na Sera za CCM, kupanga na kusimamia mafunzo na maandalizi ya makada na wanachama na kusimamia vyombo vya habari vya chama, mawasiliano na uhamasishaji wa umma. sio kitengo cha maigizo, majigambo na ngonjera za kupanda mara farasi mara sijui trekta. Itikadi ni maarifa itikadi ni maoni, anahitajika mtu atakaelewa hilo sio ujanjaujanja" Mjumbe wa NEC, jina kapuni Na. Mwandishi wetu, Katika hali isiyo ya kawaida wanachama wa chama cha mapinduzi (CCM) wamejikuta wakishangilia kuenguliwa kwa aliyekuwa katibu wa itikadi na uenezi wa chama hicho Paul Christian Makonda na kuteuliwa kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha. Makonda ambaye alitangazwa kuwa Mwenezi wa CCM Oktoba 22 mwaka jana 2023 akichukua nafasi ya Sophia mjema aliyekalia kiti hicho tangu Januari mwaka huo ambaye pia alichukua kiti hicho kutoka kwa Shaka Hamdu Shaka aliyepokea kijiti kutoka kwa Polepole alisifika kwa mbwembwe na sarakasi nyingi katika kipindi chake cha miezi mitano na wiki moja ya uenezi wake tofauti na malengo ya uwepo wa nafasi hiyo nyeti ndani ya chama hicho Katika hali isiyokuwa ya kawaida mwenezi huyo 'aliyerumbuliwa ni kama alipagawa hivi kuona ameteuliwa kuhudumu kiti hicho na kuanza kuropoka ropoka katika kila alipopanda jukwaani bila kujali aina ya hadhira "Miongoni mwa vituko vya ajabu kufanywa na mwenezi wetu huyu kwa kweli ni kutufundisha ujinga watanzania, yaani ametuambia tusiende mahakamani tukipata changamoto sasa tusipoenda mahakamani si tutauana kweli vijijini huko. Kiongozi anayetamba kukagua utekelezaji wa ilani hawezi kuropoka kijinga namna hii". Anasema Salum Kabambe mwanachama wa CCM Alipoulizwa kutoa maoni yake na gazeti hili mmoja wa wajumbe wa halimashauri kuu ya chama hicho (jina kapuni) juu ya uongozi wa makonda na kutolewa kwake alisema kuwa ameshangaa imekuwaje ameweza kufikisha hadi miezi mitano kwa kuwa siku ya kwanza tu alipozungumza na wanachama pale Lumumba alimuona kuwa hawezi kudumu kitini humo akiamini bado ana mawenge "Kwa kweli hata kumthibitisha ni kwa sababu tu tunampenda mheshimiwa Rais na kumheshimu, hivyo isingekuwa vyema kumkatalia pendekezo la huyu bwana kuwa mwenezi, wengi wetu tulijua hawezi hii nafasi". Amesema MNEC huyo "Kwa asili Mwenezi wa CCM anapaswa kuwa mtu mwenye maarifa, anayeweza kuunganisha wenzake, anayeweza kujifunza ili akafundiashe wengine, ndiye mtangazaji mkuu wa itikadi ya chama chetu, kwa hiyo ndio muuzaji hasa wa sura na roho ya CCM lazima mtu huyo asiwe mropokaji kama Makonda. Makonda ni jasiri sana akiambiwa nenda kaseme hili hapo utampenda lakini sio yeye kwenda kuanzisha na kuongoza idara muhimu kama hii". Aliongeza MNEC Alipoulizwa kama ni hivyo aliwezaje kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es salaam na sasa anaenda kuwa mkuu wa mkoa wa Arusha, alisema kuwa ukuu wa mkoa sio sawa na ukatika wa uenezi wa chama. Mtu yeyote anaweza kuwa mkuu wa mkoa lakini si kila mtu anaweza kuwa katibu mwenezi anayefaa na kuongeza kuwa hata huko Arusha akienda na mitazamo yake ile ile hatotoboa. "Idara ya Itikadi na Uenezi ni kitengo nyeti na muhimu ndani ya CCM...Miongoni mwa majukumu ya idara hiyo ni kushughulikia na kueneza masuala ya itikadi na Sera za CCM, kupanga na kusimamia mafunzo na maandalizi ya makada na wanachama na kusimamia vyombo vya habari vya chama, mawasiliano na uhamasishaji wa umma. sio kitengo cha maigizo, majigambo na ngonjera za kupanda mara farasi mara sijui trekta. Itikadi ni maarifa itikadi ni maoni, anahitajika mtu atakaelewa hilo sio ujanjaujanja" aluongeza Mjumbe huyoTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.