VICTOR MASANGU,RUFIJI
Wananchi wa wilaya ya Rufiji kata chumbi A na kata ya Muhoro Mkoa wa Pwani wamehakikishiwa kupatiwa misaada ya haraka kulingana na mahitaji ambayo wanatakiwa kupatiwa kwa kipindi hiki ambacho wameathirika kutokana na janga la mafuriko.
Kinana ameyasema hayo leo 9 , 04 ,2024 Mhe . Abdulirahmani Kinana wakati alipoenda kutoa pole kwa waathirika hao pamoja na kutoa salamu za Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassani kwa wananchi wote ambapo ameahidi kuwa ataagiza kila kinachowezekana kifanyike ili wananchi wasiendelee kuathirika .
Pia Mhe . kinana amesema kuwa nae Waziri mkuu Kassim Majaliwa tayali anashughulikia swala hilo ambapo mpaka kufikia kesho baadhi ya vifaa vitakua vimeshafika lakini kwasasa miongoni mwa vifaa vilivyopo ni pamoja na blanketi , magodoro , mahema na vyakula ila havitoshelezi kwa wahanga hao .
Aidha Makamu mwenyekiti Kinana ametumia nafasi hiyo kuwapongeza viongozi wawili ambao ni mbunge wa jimbo la ikwiriri pamoja na mbunge wa jimbo la kibiti kwakua na ushirikiano kwa wananchi wake wanaowaongoza .
Nae Mkuu wa Mkoa wa Pwani Mhe . Abubakar Kunenge amesema kuwa Maeneo ambayo yaliopatwa na athari ni jumla ya ekali elfu 34 ,na wananchi waliopata athari ni takribani kaya elfu 33 na jumla ya idadi yao ni elfu 88 lakini pia katika wilaya hiyo ya chumbi vifo vilivyopatikana ni wiwili ambavyo ni mama pamoja na mtoto .
Sambamba na hilo Mhe. kunenge ameomba kuwa miongoni mwa misaada ambayo itatolewa kwa wahanga iweze kuwafikia kwa wakati walengwa wote wenye uhitaji wa misaada hiyo .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.