ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, March 10, 2024

MCHENGERWA ATEMA CHECHE UFUNGUZI RASMI WA KAMPENI KATA YA MSANGANI

 


NA VICTOR MASANGU, KIBAHA

Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za mikoa na serikali za mitaa (TAMISEMI) Mohamed Mchengerwa amewataka wana CCM kuhakikisha kwamba wanaungana na kuwa kitu kimoja kwa lengo la kuweza kuibuka na ushindi katika uchaguzi wa kuchaza nafasi mbali mbali za udiwani katika Mkoa wa Pwani ambazo zimeachwa wazi kutokana na sababu mbali mbali.

Mchengerwa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Rufiji na mjumbe wa Halmashauri kuu ya chama cha mapinduzi (CCM) Taifa aliyasema hayo wakati wa ufunguzi rasmi wa kampeni ya udiwani katika kata ya Msangani iliyopo katika Halmashauri ya mji Kibaha.

Katika ufunguzi wa kampeni hizo ambazo ziliweza kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa CCM  kutoka katika kata zote 14 za Jimbo la Kibaha mjini pamoja na viongozi wengine kutoka ngazi ya Wilaya pamoja na Mkoa wa Pwani ikiwa sambamba na wananchi ambao waliweza kufika kwa kwa lengo lengo la kwenda kusikiliza sera za chama.

Mchengerwa alisema kwamba kwa sasa katika kuelelea chaguzi hizo inapaswa kumpa ushirikiano wa kutosha mgombea wa udiwani ili pindi atakaposhinda aweze kushirikiana na viongozi wengine katika kuwaletea wananchi chachu ya maendeleo.

"Kwa kweli tuna kila sababu kwa wana ccm wote kufanya kazi kwa bidii kuhakikisha kwamba wagombea wote waliopitishwa na chama cha mapinduzi na kupendekezwa katika vikao halali kuwashika mkono na kufanya kazi nyumba hadi nyumba kwa lengo la kuweza kuweka misingi mizuri ya kushinda kwa kishindo,"alisema Mchengrwa.

Ameongeza kwamba katika Mkoa wa Pwani kuna kata tatu ambazo kwa sasa bado zipo wazi ikiwemo kata ya Msangani hivyo ameahidi kushirikiana na wanachama wenzake katika kuelekea uchaguzi huo ili kuweza kushinda na kuwahimiza wanachama wa ccm kuwa kitu kimoja hasa katika kipindi hiki.



Kadhalika alisema kwamba hakuna sababu za kupoteza nafasi hizo kwa kata ambazo zimeachwa wazi kwani Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan ameweza kuleta mafanikio na maendeleo makubwa kwa wananchi hivyo kuna kila sababu ya kushinda kwa kishindo katika uchaguzi huo.

"tunapozungumzia maendeleo maana yangu ni kwamba Rais Samia ameweza kufanya mambo makubwa kutokana na kupeleka fedha nyingi ambazo zimekwenda katika kutekeleza miradi mbali mbali ya maendeleo katika kata ya Msangani ikiwemi miradi ya elimu, afya, miundombinu ya barabara umeme na miradi mingn=ine,"alisema Mchengerwa.

Pia Mchengerwa alisema kwamba viongozi wa CCM pamoja na diwani wa kata ya Msangani ambaye atachaguliwa katika uchagauzi huo wanatakiwa kuwafikia wananchi kwa wakati kwa kuhakikisha kwamba  wanakwenda kusikiliza kero mbai mbali ambazo zinawakabili wananchi ili kuweza kuzitafutia ufumbuzi.

"ndugu zangu nimekuja hapa kata ya Msangani lakini kitu kikubwa nawataka viongozi wa ccm hsa wale wa kuchaguliwa kufanya kazi kwa bidii na kuhakikisha wanatetea maslahi ya wananchi wake na sio kwa ajili ya matumbo yao binafsi na hili jambo ni muhimu sana ndio maana nimewaambia,"alisema Mchengerwa.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mji mwalimu Mwajuma Nyamka  alisema  kwamba  viongozi  na wanachama wa ccm  wanatakiwa  kuvunja kabisa makundi yote na kuhakikisha wanakuwa kitu komoja kwa ajili ya kukiimarisha chama kuanizia ngazi za chini hadi za juu.

Naye mgombea wa nafasi ya udiwani katika kata ya Msangani Gunze Yohana amewahidi wananchi wa Msangani pindi atakoshinda katika uchaguzi huo kushirikiana nao bega kwa bega katika kuwasikiliza kero mbali mbali zinazowakabili ili aweze kuzifanyia kazi na kuzitatua.

Kadhalika aliongeza kuwa changamoto ambazo zinawakabili wananchi wa Msangani anazitambua vizuri hivyo ana imani kubwa endapo akiweza kuchaguliwa atazichukua kwa kuzishughulikia kwa haraka ikiwa pamoja na kuleta miradi mbali mbali ya maendeleo ambayo itaweza kugusa katika nyanja mbali mbali.

Uchaguzi wa kujaza nafasi ya udiwani katika kata ya Msangani katika halmashauri ya mji Kibaha pamoja na maeneo mengine yaliyokuwa wazi unatarajiwa kufanyika mwezi machi mwaka huu katika Wilaya tatu za Mkoa wa Pwani ambazo zilikuwa zimeachwa wazi kutokana na sababu mbali mbali.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.