VICTOR MASANGU,KIBAHA
Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kibaha mjini Mwalimu Mwajuma Nyamka amempongeza Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo kutekeza miradi pamoja na kuwatumikia wananchi katika nyanja mbali mbali.
Akizungumza na mwandishi wa habari katika mahojiano maalumu kuhusiana na maadhimisho ya miaka 47 ya kuzaliwa kwa chama cha mapindu CCM.
Mwalimu nyamka akitolea ufafanuzi zaidi alisema kwamba wananchi na wanachama wanatakiwa kutambua kwamba chama chama cha mapinduzi kimetokana na muunganiko wa chama cha TANU kwa upande wa Tanzania bara na chama cha ASP kwa upande wa Zanzibar.
"Kwa hiyo vyama hivi viliweza kuungana kwa pamoja ndipo vikaunda chama cha mapinduzi kwa hivyo ni vizuri watu wakaelewa zaidi kupitia maadhimisho haya ya miaka 47 ya kumbukizi ya CCM,"alifafanua Mwalimu Nyamka.
Kadhalika alisema kuwa baadhi ya watu hawafamu chama cha mapinduzi kimetokana na nini hivyo kupitia maadhimisho haya ya miaka 47 wataweza kuelewa zaidi kuhusiana na CCM ilipotoka na hadi ilipo kwa sasa.
"Unapozungumzia chama cha TANU kipindi kile kirefu chake ni Tanganyika African Nation Union ambacho kilikuwa kinaongozwa na hayati Baba wa Taifa Mwalimu Julias Kambarage Nyerere,"
Kadhalika Nyamaka aliongeza kwamba chama cha mapinduzi kimeunganishwa mnamo tarehe 5 mwezi wa 2 mwaka 1977 ambapo sasa chama ndio kinatimiza miaka 47,"alifafanua Mwalimu Nyamka.
Pia alisema kwamba katika kipindi chote cha miaka 47 chama cha mapinduzi kimeweza kufanya mambo mengi sana ikiwemo katika suala la utawala pamoja na utekelezaji wa Ilani.
"Utekelezaji wa Ilani ya Chama cha mapinduzi CCM ni moja ya mkataba na wananchi katika kusimamia mambo mbali mbali na kwamba ilani inasimamiwa vizuri sana na Mama yetu Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan,"alisema Nyamka
Katika hatua nyingine Mwalimu nyamka alipongeza kwa dhati Rais wa awamu ya sita Dkt.Samia Suluhu Hassan kwa kutekeleza ilani ya CCM kwa vitendo pamoja na kuwatumikia wananchi wake kuanzia kwa mtu mmoja mmoja hadi makundi kwa njia tofauti.
Aliongeza kwamba Rais Samia ameweza kutoa fedha nyingi kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbali mbali ya kimaendeleo ikiwemo Afya,Elimu,umeme,miundombinu ya barabara,maji pamoja na maeneo mengine amefanya mambo makubwa hivyo anastahili pongezi.
Katika kutekeleza Ilani ya chama kwa vitendo Rais Samia ameweza kuwakomboa wakinamama kuondokana na kutembea umbari mrefu kwa ajili ya kutafuta huduma ya maji na kupelekea kutimiza dhamira yake ya kumtua mama ndoo ya maji kichwani.
Katika hatua nyingine Mwenyekiti huyo alisema katika kuelekea uchaguzi wa serikali za mitaa ambao utafanyika mwaka huu watahakikisha wanashinda kwa kishindo na kwamba watatembea kifua mbele kutokana na kuwa na sababu za msingi za kuwaeleza wananchi.
Maadhimisho ya kuzaliwa kwa miaka 47 ya chama cha mapinduzi (CCM) yameambatana na shughuli mbali mbali za kijamii ambazo zimefanyika katika maeneo mbali mbali ya Mkoa mzima wa Pwani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.