Na Victor Masangu,Kibaha
Mke wa Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Selina koka katika kuunga mkono juhudi za Rais wa awamu ya sita Dkt. Samia Suluhu Hassan kàtika kuboresha sekta ya elimu ametoa viti na meza 16 katika shule ya msingi Mwanalugali kwa ajili ya kuwasaidia walimu kukaa katika mazingira ambayo ni rafiki.
Selina amesema kwamba lengo lake kubwa ni kuboresha sekta ya elimu hivyo ameamua kutoa viti hivyo ambavyo vitaweza kuwasaidia walimu katika kutimiza majukumu yao ipasavyo na kuondokana na changamoto ambayo walikuwa wanaipata.
Alisema kwamba hatua hiyo ya kutoa viti hivyo ni kutokana na risala ambayo ilitolewa hivi karibuni wakati wa mahafali ya shule ambapo walibainisha changamoto zao mbali mbali ambazo zinaikabili shule hiyo ikiwemo uhaba wa viti.
Aidha mbali na kutoa viti hivyo ametoa vifaa mbali mbali kwa ajili ya kufanyia usafi vikiwemo mafagio,sabuni za maji sulari,pamoja na fedha kiasi cha shilingi laki mbili kwa ajili kununua unga kwa ajili ya wanafunzi.
Aidha alibainisha kwamba vifaaa hivyo vitaweza kuwapa fursa ya shule hiyo kuboresha mazingira ya shule hiyo yawe katika hali ya usafi.
"Nimefika katika shule ya msingi ya Mwanalugali na nimetoa vifaa mbali mbali ikiwemo viti 16,vifaa vya usafi vikiwemo sabuni pamoja na mafagio ya nje pamoja na mafagio ya ndani na hii yote ni katika kuweka mazingira mazuri kwa wanafunzi na walimu,alisema Selina.
Kwa upande wake Diwani wa kata ya Tumbi mhe.Chokara alimpongeza Mama Selina Koka kwa juhudi zake za kuchangia katika sekta ya elimu na kuleta matokeo chanya katika kuchagiza maendeleo katika nyanja mbali mbali na kuwa karibu katika kuwasaidia wananchi.
Naye Mwenyekiti wa shule ya msingi Mwanalugali amemshukuru mke wa Mbunge Selina Koka kwa kutekeleza ahadi hiyo kwa vitendo kwa kutoa viti hivyo kwa ajili ya walimu.
Katibu wa jumuiya ya wazazi Mkoa wa Pwani alisema Selina Koka amekuwa mstari wa mbele katika kushirikiana na wananchi wa Jimbo la Kibaha katia kutekeleza miradi mbali.mbali ya maendeleo.
Alisisitiza kwamba wananchi wanapaswa kuwa na ushirikiano na Mbunge wao lengo ikiwa ni kuleta mabadiliko katika nyanja mbali mbali ikiwemo elimu pamoja na mambo mengine.
Kaimu Mwalimu mkuu wa shule hiyo ya Mwanalugali amempongeza kwa dhati mke wa Mbunge Selina Koka kwa kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya sita katika kuboresha sekta ya elimu.
Nao baadhi ya wazazi waliohudhulia katika halfa hiyo fupi nao hawakusita kutoa shukrani zao kwa msaada ambao ameweza kuutoa katika shule hiyo ikiwemo sukari,meza.mafagio pamoja na fedha
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.