ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, July 17, 2023

SHULE MPYA YA SEKONDARI KUJENGWA KIBAHA KUWAEPUSHA WANAFUNZI KUSAFIRI UMBALI MREFU.

 VICTOR MASANGU,PWANI


Hatimaye kilio cha siku nyingi kilichokuwa kinawakabili baadhi ya wanafunzi wa shule ya sekondari nyumbu ya  kutembea umbari mrefu wa kilometa 18 wanatarajia kuondokana na adha hiyo baada ya serikali kutoa shilingi milioni 528 kwa ajili ya ujenzi wa shule mpya itakayojengwa eneo la Mbwate  kata ya mkuza Wilayani Kibaha.

Hayo yamebainishwa na Diwani wa Kata ya Mkuza wakati akitoa taarifa katika halfa maalumu iliyoandaliwa kwa ajili ya uzinduzi rasmi wa eneo lenye ukumbwa wa  hekari tano ambalo limetemgwa  kwa matumizi ya utekelezaji wa mradi huo wa ujenzi wa shule ya sekondari.

Kwa Upande wake Afisa elimu sekondari katika halmashauri ya Kibaha mji amesema tayari serikali imeshatoa fedha hivyo kilichobaki ni kuanza ujenzi haraka ili wanafunzi waondokane kabisa  na mateso ya kutembea umbari mrefu kufuata huduma elimu.

Naye Mbunge wa Jimbo la Kibaha mjini Silvestry Koka ambaye aliungana na wananchi katika uzinduzi wa mradi huo amechangia kiasi cha shilingi milioni moja ikiwa ni kuchochea zaidi katika kuboresha sekta ya elimu.

Wanafunzi wa shule ya sekondari nyumbu iliyopo kata ya Mkuza Wilayani Kibaha wamekuwa wakisumbuka kwa kipindi kirefu cha kutembea umbari mrefu kufuata masomo yao hivyo kukamilika kwa ujenzi huo utakuwa ni mkombozi mkubwa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.