ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, July 18, 2023

NYANZA BOTLING WAPOKEA MAGARI 10 KATI YA MAGARI 150 YA MKOPO WA NGUVU KUTOKA EFTA

 NA ALBERT G.SENGO/MWANZA

Ili kuweza kufanikisha utoaji wa huduma na usambazaji wa bidhaa zake Kanda ya Ziwa Victoria, kampuni ya kutengeneza vinywaji ya Nyanza Bottling Company Limited ya Igoma Jijini Mwanza leo hii imepokea magari 10 kati ya 150 ya mkopo kutoka kwa Taasisi ya fedha ya EFTA.
Kwa mujibu wa Japhet Kisusi ambaye ni Mkuu wa Idara ya Mauzo na Masoko Nyanza Bottling Co Ltd anasema magari hayo yanakwenda kusukuma kasi ya usambazaji wa bidhaa za kampuni yake kulingana na mahitaji ya soko kwani awali kabla ya ujio wa magari hayo sekta ya usafirishaji ilikuwa ikikabiliwa na changamoto. Mbali na wafanyabiashara na wawekezaji sekta ya madini wakulima nao ni moja kati ya wanufaika wa mikopo ya EFTA ambapo kwa mwaka mmoja wa 2022 wakulima wapatao 330 kutoka maeneo mbalimbali nchini, walipata mkopo wa trekta kupitia mpango wa matumizi bora ya zana za kilimo na fedha unaoendeshwa na Taasisi hiyo ya Fedha (EFTA) iliyo chini ya Benki Kuu ya Tanzania.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.