Mbunge wa Jimbo La Kilolo Justine Nyamoga akimshukuru Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Nancy Nyalusi kwa kuchangia shilingi millioni kumi kwaajili ya kuanza ujenzi wa jengo la mama na mtoto katika kijiji cha Kimala wilya ya Kilolo
Na Fredy Mgunda,Kilolo
Mbunge wa Jimbo La Kilolo Mhe Justine Nyamoga amemshukuru Mbunge wa Viti Maalumu Mkoa wa Iringa Mhe Nancy Nyalusi wa kuchangia shilingi millioni kumi kwaajili ya kuanza ujenzi wa jengo la mama na mtoto.
Nyamoga amemshukuru nyalusi leo katika kijiji cha kimala kata ya kimala wakati akifanya mkutano na wananchi wa kijiji hicho ambapo hadi sasa wamama wajawazito walikuwa wanaenda umbali mrefu kwaajili ya kupata huduma
“ Poleni sana wanakijiji wa kijiji cha Kimala kwa kupata changamoto hii ya kwenda umbali mrefu hadi Kidabaga kwaajili ya kupata huduma mimi nitatoa shilingi milioni kumi kwaajili ya ujenzi wa zahanati na naomba ujenzi huu uanze mara moja kwasababu fedha sasa ipo “ Amesema Nyalusi
Hatahivyo Nyamoga amewataka wananchi waweze kushiriki katika ujenzi wa zahanati hiyo ili ijengwe kwa haraka sana ili iweze kuwa msaada kwa kina mama
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.