June Jerop, mwanafunzi wa chuo kikuu cha Kenyatta aliyekuwa akisomea shahada ya uzamili katika Utawala wa Biashara alipatikana akiwa amefariki saa chache baada ya kwenda kuchumbiana na jamaa anayeshukiwa kuwa mpenzi wake.
June Jerop,
36 alikaa siku nzima na marafiki zake mnamo Machi 18 kabla ya kujiondoa kwenda
kwenye mtoko huo. Aliwaambia rafikize kuwa atakutana na rafiki wa kiume kwenye
mgahawa mahali flani lakini hakufichua mengi kuhusu hilo.
Baada ya
mtoko huo simu yake ilizima na familia yake na marafiki walijaribu kuwasiliana naye
bila mafanikio.
Mwili wake
uliripotiwa kutupwa karibu na Shule ya Msingi ya Jamhuri jijini Nairobi kabla
ya polisi kuhamishia mwili wake katika chumba cha kuhifadhi maiti cha City.
Kulingana na polisi, mwili wake ulipatikana ukiwa umevimba na ukiwa na damu.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.