NA ALBERT G.SENGO/MWANZA
Mbunge wa zamani wa Tarime Vijijini, John Heche ameendelea kuwachongea kwa Rais Samia Suluhu Hassan, Mawaziri, viongozi na watendaji wa wizara, mashirika na taasisi za umma zinazotajwa katika ripoti ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG) akitaka wawajibishwe. Heche ambaye pia ni Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chadema amemshauri Rais Samia kuanza kwa kuiwajibisha kwa kuiondoa ofisini manejimenti ya Shirika la Reli nchini (TRC) kama alivyofanya kwa Bodi ya Wakurugenzi wa shirika hilo baada ya ripoti ya CAG kuibua kashfa ya hasara ya Sh1.7 trilioni kwa kutoa zabuni bila ushindani.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.