NA ALBERT G. SENGO
"Kama inspekta Jenerali wa polisi sijakubali maandamano yoyote. Hiyo ni mizozo ya kisisasa na inafaa kusuluhishwa bila kuingilia na kuvuruga amani ya nchi' asema Inspekta Jenerali wa Polisi nchini Kenya Japhet Koome Katika matamshi yalionekana kumlenga Raila, Koome alisema maafisa wake watamkamata yeyote ambaye atashiriki maandamano yaliyoharamishwa bila kujali wadhifa wao katika jamii. Wakati kauli hiyo inatoka tayari kiongozi wa Azimio la Umoja Raila Odinga amemtaka Inspekta Koome kumkamata kuhusiana na maandamano yaliyopangwa dhidi ya serikali. Akimjibu Koome Jumapili (leo) Machi 26, kiongozi huyo wa ODM amesema kuwa maandamano yake ni ya amani na yataendelea kama ilivyopangwa yaani Jumatatu, Machi 27. Raila aliteta kuwa tayari alikuwa ametoa notisi ya maandamano kulingana na Katiba. Waziri Mkuu huyo wa zamani alimtaka Koome amkamate yeye binafsi, akithibitisha atakuwa kwenye mstari wa mbele katika maandamano hayo. "Bwana Koome, Koma kabisa. Unasema ati unaweza shika kila mtu, mimi niko tayari, nitakuwa kwa mstari wa mbele, Koome hapana tuma askari njoo wewe mwenyewe tuonane ana kwa ana," alisema Raila.Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.