Mamia ya watu wasiojulikana wamevamia shamba la familia ya rais wa zamani wa Kenya Uhuru Kenyatta huku maandamano yakizuka nchini humo kuhusu gharama ya juu ya maisha.
Wavamizi hao
walikata miti Kwa kutumia misumeno ya umeme na kuiba mamia ya mifugo kutoka kwa
shamba kubwa lililo nje kidogo ya jiji kuu la Nairobi.
Sehemu kubwa ya
ardhi imetengwa kwa ajili ya mradi wa makazi ya hali ya juu. Hakukuwa na polisi
au vikosi vya usalama kwenye eneo hilo . Waandishi wa habari wa eneo hilo
wanaoripoti uvamizi huo pia walishambuliwa na umati huo.
Biashara karibu
na shamba lote zimefungwa. Kiwanda cha gesi kinachomilikiwa na familia ya
kiongozi wa upinzani Raila Odinga pia kimeharibiwa katika eneo la viwanda la
Nairobi.
Maandamano pia
yamefanyika katika miji na majiji kote Magharibi mwa Kenya, ngome ya Bw Odinga.
Waandamanaji walichoma matairi na kuziba barabara kuu katika jiji la Kisumu.
Takriban
muandamanaji mmoja ameuawa katika ghasia hizo.
Bw Odinga,
aliitisha maandamano nchi nzima kuhusu madai kuwa uchaguzi wa mwaka jana
uliibiwa.
Pia anasema
rais William Ruto ameshindwa kushughulikia gharama ya juu ya maisha nchini.
Raila,
aliyekuwa Waziri Mkuu alishindwa na Bw Ruto katika uchaguzi wa Agosti mwaka
jana. Aliungwa mkono na aliyekuwa rais Uhuru Kenyata
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.