ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, February 13, 2023

CHANGAMOTO ZA UCHUMI ZINAZOVIKABILI VYOMBO VYA HABARI NCHINI TAYARI SERIKALI IMECHUKUWA HATUA.

 NA ALBERT G. SENGO/DODOMA

Kwa kutambua changamoto za kiuchumi zinazovikabili vyombo vya habari nchini likiwemo suala la kusuasua katika uendeshaji, Serikali ya Tanzania imechukuwa hatua ya kupunguza ada za mwaka za leseni za utangazaji kwa takriban asilimia 40. Naibu Waziri Wizara ya Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Eng. Kundo A. Mathew amesema hayo hii leo jijini Dodoma, katika Mkutano wa Mwaka wa Watoa Huduma wa Sekta ya Utangazaji Tanzania ikiwa ni maadhimisho ya Siku ya Redio Duniani. Aidha Eng. Kundo amesema kuwa Serikali imepunguza ada za masafa ya utangazaji maeneo ambayo hayana tija kibiashara. "Hatua hii yote ni dhamira safi ya Serikali ya Awamu ya sita chini ya Dkt. Samia Suluhu Hassan kuhakikisha kuwa huduma za utangazaji zinaboreshwa" alisema Kundo. ................................................................................................ Siku ya Redio Duniani, huadhimishwa kila mwaka ifikapo Februari 13 kuashiria nafasi muhimu ambayo redio inatekeleza wajibu wa kutuhabarisha katika maisha yetu ya kila siku katika jamii. Siku hii ilianzishwa na Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa mwaka 2012, na historia yake ilianza kufuatiliwa kwenye Mkutano wa kwanza wa Kimataifa wa Redio huko Geneva mwaka 1974 na ilitangaza Februari 13 kuwa Siku ya Redio Duniani kwa sababu tarehe hii ndiyo Redio ya Umoja wa Mataifa ilianzishwa kwa mara ya kwanza mwaka 1946. Kwa kuona umuhimu wa redio, na pia kuhimiza wafanya maamuzi kutoa upatikanaji wa Habari kupitia redio, UNESCO inaratibu shughuli za Siku ya Redio Duniani kwa kiwango cha kimataifa na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa, kupitia vituo vyao vya redio.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.