ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 29, 2022

WAZIRI ATEMBELEA MRADI WA MAJI KISARAWE AWAFUNDA WATUMISHI WA DAWASA KUJIKITA KUSAMBAZA MAJI.


Na Victor Masangu,Pwani

Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ameiagiza mamlaka ya maji Safi na usafi wa mazingira (DAWASA) kuhahakikisha wanaweka mifumo mizuri ya kuhifadhi na  kusambazàji wa  huduma ya maji kwa wananchi ili kupunguza kero na vilio vinavyotokea pindi ukame wa maji unapotokea na kusabisha adha kubwa.


Majaliwa ametoa kauli hiyo wakati wa ziara yake ya kikazi Wilayani Kisarawe mkoa wa pwani yenye lengo ya kugagua miradi mbali mbali ya kimaendeleo huku akiwatoa hofu wananchi juu ya upatikanaji wa maji kwani ameridhishwa na upatikanaji mzuri wa maji uliopo kwa Sasa na utendaji wa dawasa katika kutoa huduma ya maji.

Alisema kwamba watumishi wa dawasa wanapaswa kuendelea kutekeleza majukumu yao ipasavyo kwa kuhakikisha wanasambaza huduma ya maji kwa wananchi ili waweze kuondokana na changamoto ya maji.


"Nipo katika ziara katika Mkoa wa Pwani na leo nipo Wilayani Kisarawe na nimetembelea miradi mbali mbali ukiwemo mradi mkubwa wa maji na dawasa wanafanya kazi nzuri na nimeridhishwa na upatilanaji wa maji katika mkoa wa Dar es Salaam na Pwani,"alisema Majaliwa.


Pia Majaliwa aliitaka dawasa kuhakikisha kwamba wanaweka mipango mizuri ya kuvitunza vizuri visima ambavyo wamevichimba ambavyo vitaweza kusaidia kwa kiasi kikubwa hasa katika kipindi cha kiangazi.

Kwa upande wake Waziri wa nchi ofisi ya Makamu wa Rais  muungano na mazingira ameipongeza serikali kwa kutenga zaidi ya bilioni 10 kwa ajili ya  kutatua kero sugu ya upatikanaji wa maji Safi na salama huku akiomba kupelekwa maji katika kata tano ambazo bado zina shida ya maji.


Aidha Waziri jafo alibainisha katika kipindi cha miaka ya  nyuma wilaya ya Kisarawe kulikuwa na changamoto kubwa ya ukosefu wa maji lakini kwa sasa wananchi wamenufaika baada ya mradi huo mkubwa kukamilika.

Naye mtendaji mkuu wa Dawasa amesema kwamba kwa sasa kiwango cha hali ya upatikanaji wa maji kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani na Dar es Salaam kimeongezeka kwa kiasi kikubwa kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha.

Aidha Luhemeja aliongeza kwamba lengo lao kubwa ni kuwahudumia wananchi katika maeneo mbali mbali kwa kuwapatia huduma bora ya maji safi na salama na kuahidi kuendelea kusambaza maji kwa wananchi.


Waziri mkuu amehitimisha ziara yake ya siku tatu katika Wilaya ya Kisarawe Mkoa wa Pwani ambapo leo ametembelea  na kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo katika sekta ya elimu,afya pamoja na maji.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.