ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Thursday, November 10, 2022

SERIKALI KUCHUNGUZA MWENENDO WA MIKOPO YA HALMASHAURI

 

Serikali imeunda timu ya uchunguzi kufuatilia mikopo ya asilimia kumi inayotolewa kwa vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu ili kubaini ikiwa fedha hizo zinawanufaisha walengwa.

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki amebainisha hayo Alhamisi Novemba 10, 2022 jijini Dodoma wakati akifunga kikao kazi cha Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Waziri Kairuki amesema baada ya uchunguzi huo kukamilika, Serikali itachukua hatua za kisheria dhidi ya wote watakaobainika kukiuka kanuni, taratibu na sheria za utoaji wa mikopo hiyo ikiwemo kuanzisha vikundi hewa.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainabu Chaula amewataka maafisa maendeleo ya jamii kusimamia vyema majukumu yao ikiwa ni pamoja na kuhakikisha mikopo inayotolewa na halmashauri inaleta tija kwa walengwa.

Kwa upande wake mdau wa maendeleo, Yassin Ally ambaye ni Mkurugenzi Mtendaji wa shirika la kutetea haki za wanawake na watoto KIVULINI amesema usimamizi mzuri wa mikopo inayotolewa na halmashauri nchini utaimarisha kiwango cha uchumi wa kaya na hivyo kupunguza vitendo vya ukatili dhidi ya wanawake na watoto.
Na George Binagi-GB Pazzo, BMG
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, Angellah Kairuki akihitimisha kikao kazi cha maafisa maendeleo ya jamii jijini Mwanza.
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Zainabu Chaula akizungumza kwenye kikao hicho.
Mkurugenzi Mtendaji Shirika la KIVULINI, Yassin Ally akichagiza mada kwenye kikao hicho.
Maafisa Maendeleo ya Jamii wakiwa kwenye kikao hicho.
Washiriki wakifuatilia kikao hicho.
Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Sekretarieti za Mikoa na Wakuu wa Idara za Mamlaka za Serikali za Mitaa wakiwa kwenye kikao kazi cha siku tatu kuanzia Novemba 08-10, 2022 jijini Dodoma.
Picha ya pamoja.
Tazama BMG TV hapa chini

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.