Dar es Salaam. Watu kadhaa wanahofiwa kujeruhiwa kutokana na ajali iliyohusisha magari matatu iliyotokea eneo la Kitengule Tegema jijini Dar es Salaam leo Novemba 11, 2022.
Kamanda wa polisi mkoa wa Kinondoni, Mtatiro Kitinkwi amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo alipoulizwa kwa simu, hata hivyo amesema taarifa zaidi atazitoa kwani kwa sasa yupo nje ya ofisi.
“Nilikuwa nje ya ofisi kikazi ndiyo ninarudi, lakini hilo tukio lipo na limetokea…nikirudi ofisi nikiiandaa basi nitatoa taarifa,” amesema kamanda huyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.