Ndege ya Shirika la Precision Air imepata ajali katika Ziwa Victoria, muda mfupi kabla ya kutua mjini Bukoba mkoani Kagera.
Akizungumza toka eneo la tukio leo Jumapili 6, 2022, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kagera, William Mwampaghale amethibitisha taarifa za ajali hiyo na kusema kuwa yupo kwenye eneo la tukio akiendelea na uokoiaji.
“Iko sahihi hiyo taarifa niko kwenye eneo la tukio nafanya uokozio, wananchi wawe na subira tutatoa taarifa zaidi kwa kina” amejibu kwa kifupi Kamanda Mwampaghale .
Taarifa za awali zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii zimeonyesha ndege hiyo ikiwa imetumbukia kwenye maji huku ikiwa imezungukwa na mitumbwi nao baadhi ya watu wakiwa ukingoni mwa ziwa wakifuatilia tukio hilo.
Ndege hiyo imepata ajali mita 100 hatua chache kabla ya kutua Uwanja wa Ndege wa Bukoba ikitokea jijini Dar es salaam, na ilikuwa ikitazamiwa kuelekea jijini Mwanza.
Bado haijajulikana idadi ya abiria waliokuwa ndani ya ndege hiyo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.