ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Sunday, October 30, 2022

PENALTY HAITUHUSU | TAMBO ZA 'KIGEREGERE YANGA' BAADA YA YANGA KUPATA USHINDI DHIDI YA GEITA GOLD.

 DAKIKA 90 za jasho zimekamilika Uwanja wa CCM Kirumba ambapo ubao umesoma Geita Gold 0-1 Yanga.

Bao pekee la ushindi limefungwa na kiungo Bernard Morrison kwa pigo la penalti dakika ya 45. Penalti hiyo imezua gumzo kwa wachezaji kutokana na mazingira yake ilivyopatikana na mwamuzi wa kati kuamua lipigwe tuta. Jitihada za Geita Gold kupata bao wakiwa na kiungo wao Said Ntibanzokiza aliyechomoka Yanga msimu uliopita, ziligonga mwamba na kuwafanya wapoteze pointi tatu mazima. Yanga inafikisha mechi 45 za Ligi Kuu Bara bila kupoteza tangu msimu wa 2021/22. Kigeregere Yanga ni mmoja wa mashabiki wakubwa akitumia style yake ya kuchagiza na kutia hamasa kwa kutumia mruz, msikilize huyu hapa.




Jibu la Wakili msomi 💬 "Kukataa kupiga penati iliyoamuliwa na refa ni makosa MAKUBWA katika sheria na kanuni za mpira uwanjani. Ni sawa na kuoneshwa kadi nyekundu halafu ukagoma kutoka uwanjani" "Kazi yetu uwanjani ni kucheza mpira na kumsikiliza mwamuzi aliyesomea kutafsiri kanuni na sheria. Sio kazi yetu kujua mwamuzi yuko sawa au laa, maana yeye ndiye alienda darasani kwa kazi hiyo kama sisi tunavyovuja jasho katika viwanja vya mazoezi kuelewa namna ya kucheza" "Cha msingi kila mmoja ajitahidi kuwa bora katika eneo la taaluma yake kama sisi tulivyoamua kuwa bora kutofungwa (UNBEATEN), pia kufunga penati kwa UBORA MKUBWA" 🔍 Bernard Morrison

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.