Jayo yameelezwa na Mwenyekiti wa halmashauri ya Wilaya ya Tabora, Said Ntahondo akisema kiongozi huyo alikuwa pia akienda kuhudhuria kikao cha CCM.
Amesema alikuwa na kawaida ya kwenda mjini Tabora kurahisisha safari ya kwenda Isikizya umbali wa kilometa 40 kutoka mjini Tabora yalipo makao makuu ya wilaya ya Uyui.
"Leo tulikuwa tunaanza vikao vyetu na kikao cha chama kilikuwa kianze na Baraza la Madiwani kesho Jumatano," amesema.
Amesema alipata taarifa za ajali hiyo kupitia mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Tabora,Hassan Wakasuvi ambaye alimweleza kutokea ajali hiyo na diwani kufariki.
Ameeleza kuwa walienda eneo la tukio usiku huo na kukuta miili ya marehemu ambayo waliichukua na kuipeleka hospitali ya Kitete kwa ajili ya kuihifadhi na taratibu zingine.
Amesema bado wanasubiri taratibu za kiuchunguzi kwani madaktari wanaendelea na taratibu zao na wakimaliza,wataichukua miili kwa ajili ya maziko saa kumi leo.
Katibu wa CCM wilaya ya Uyui, Bakari Mfaume,amesema chama kimempoteza diwani wake muhimu ambaye ameacha pengo kutokana na kuwatumikia wananchi wake kwa uadilifu mkubwa.
Amesema.chama kipo na familia ya marehemu katika majonzi na kipindi hiki kigumu kwao na kwamba kitatoa ushirikiano unaohitajika.
Diwani Sauji Daud Sauji na mkewe, Magdalena walifariki katika ajali ya gari usiku wa kuamkia leo eneo la Ulimakafu,wilayani Uyui.
Kamanda wa Polisi mkoa wa Tabora,Richard Abwao, alipoulizwa kuhusu ajali hiyo, amesema yupo Dodoma akiwa njiani kurudi Tabora na kwamba anatarajia kufika saa tisa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.