Mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan Moyo ametoa siku saba
kwa mawakala wa pembejeo za kilimo kufikisha mbole aina zote kwa wakulima huku
wakisubili serikali kutatua changamoto za kimfumo ambazo wanakabiliana nazo.
Akizungumza wakati kikao kazi na wadau,mawakala na kampuni
zinazosambaza mbole katika Halmashauri ya Manispaa ya Iringa,mkuu wa wilaya
Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wakulima wamekuwa wanalalamika kuwa mbolea
haziwafikii mahali walipo kutokana na mawakala kutopeleka mbolea hizo maeneo husika.
Moyo alisema kuwa serikali ilishatangaza kuwa wananchi wote
waliojiandikisha wanatakiwa kununua mbolea kwa bei ya chini kutokana na
serikali kuweka fedha ya ruzuku kwenye kila mfuko wa mbolea ambao mkulima
anataka kununua.
Alisema kuwa anatambua kunachangamoto ya kimfumo kutokana na
teknolojia ambayo wanaitumia wizara hivyo atawasilisha malalamiko hayo sehemu
husika ili watatue changamoto hiyo na wakulima waweze kupata mbolea kwa muda
ambao unatakiwa.
Moyo alisisitiza kuwa kampuni, mawakala na wadau wa pembejeo za
kilimo lazima wazipeleke pembejeo hizo kwa wakulima kwa kuwa wamekuwa
wanafanyabiashara ambayo inawalipa na wanapata faida.
Alimazia kwa makampuni ya STACCO Tanzania,YARA Tanzania, PREMIUM
Tanzania,OCP Tanzania na E.T.G Tanzania yanatakiwa kuongeza idadi ya mawakala
wa kusambaza mbolea kwa wakulima ili waweze kuanza maandalizi ya Kilimo.
Awali akitoa taarifa kwa mkuu wa wilaya ya Iringa Mohamed Hassan
Moyo, afisa kilimo Halmashauri ya Manispaa ya Iringa Victor Kilatu alisema kuwa
baadhi ya mawakala walioteuliwa kuuza pembejeo za ruzuku kutouza pembejeo kwa
sababu hawajapewa uwezo wa kuingia kwenye mfumo jambo ambalo linawafanya
wachelewe kufikisha mbolea kwa wakulima.
Kilatu alisema kuwa kunachangamoto kubwa ya makampuni kushindwa
kuwateua mawakala wa kuuza pembejeo na kusababisha kuwa na idadi ndogo ya
mawakala ambao wanauza pembejeo za ruzuku jambo ambalo linapelekea
kucheleweshwa kwa pembejeo hizo kufika kwa wakulima.
Kwa viongozi wa makampuni ya kusambaza
pembejeo za mbolea STACCO Tanzania,YARA Tanzania, PREMIUM Tanzania,OCP Tanzania
na E.T.G Tanzania waliiomba
serikali kulipa fedha mapema waendelee kusambaza pembejeo hizo.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.