ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, August 10, 2022

FIFA KUENDELEA KUISAIDIA TANZANIA, YALIDHISHWA NA UTENDAJI WA RAIS SAMIA

 

Na John Mapepele

Rais wa Shirikisho la Soka Duniani(FIFA) Gianni Infantino  amesema  FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania kutokana na kuridhishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Serikali inayoongozwa na Rais Samia Suluhu Hassan kwenye Michezo.

Akizungumza usiku wa kuamkia leo Agosti 10, 2022 mara baada ya kupokelewa na Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe Mohamed Mchengerwa katika kiwanja cha ndege cha Kilimanjaro amesisitiza kuwa FIFA itaendelea kuisaidia Tanzania.

Akiongozana na wachezaji mahiri wazamani waliopata kucheza katika makombe ya dunia na mwamuzi  Corina amesema amefurahishwa na jitihada mbalimbali zinazofanywa na Tanzania.

"Tayari FIFA imekwishatoa msaada wa ujenzi wa viwanja changamani Dar na Tanga lakini wako tayari kwa ajili ya kuongeza vituo katika kanda nyingine" amefafanua Mhe. Mchengerwa

Aidha, Mhe. Mchengerwa amemshukuru Mhe. Rais Samia Suluhu Hassan kwa jitihada kubwa kwenye ambayo imesaidia Tanzania kupiga hatua duniani katika michezo.

Mhe. Mchengerwa amepokea viongozi mbalimbali wa juu kwenye mashirikisho ya Soka duniani na kufanya  vikao vya kuendeleza michezo ambao leo wanahudhuria mkutano Mkuu wa 44 wa Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) jijini Arusha.

Aidha, Mhe. Mchengerwa ametumia fursa hiyo kuendelea kuimarisha mahusiano na mashirikiano na nchi mbalimbali ambazo tayari ziliahidi kuendeleza mashirikiano katika sekta za michezo, Sanaa na Utamaduni.

Mkutano huu wa kihistoria unatarajiwa kuhudhuria na zaidi ya watu mia tano na waandishi wa habari zaidi ya mia moja huku ikitarajiwa kuangaliwa na zaidi ya watu bilioni moja.

Tayari viongozi  wakuu wa mashirikisho yote ya Soka kutoka mabara yote wamewasili na Waziri Mkuu, Mhe. Kassimu Majaliwa  anatarajiwa kumwakilisha Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe Samia Suluhu Hassan.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.