Waziri wa nishati January Makamba akiongea na wadau wa nguzo za umeme mkoani Iringa akiwaondolea sitofaumu iliyokuwepo ya kutonunua nguzo zaoWaziri wa nishati January Makamba akiwasikiliza wadau wa nguzo za umeme mkoani Iringa akiwaondolea sitofaumu iliyokuwepo ya kutonunua nguzo zaoWaziri wa nishati January Makambaakiteta jambo na Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga wakati wa majadiliano ya kuondoa sitofaumu iliyokuwepo ya kutonunua nguzo zao
Na Fredy Mgunda,Iringa.
WAZIRI wa nishati January Makamba ameliagiza shirika la umeme Tanzania (TANESCO) kuingia zabuni za ununuzi wa nguzo za kusambaza umeme kwa wakandarasi wanaokidhi vigezo,ikiwemo kuthibitisha baadhi ya nguzo zimetoka kwa wazalishaji wadogo wa ndani.
Waziri Makamba alisema kuwa TANESCO inatakiwa kushirikiana na taasisi zinazosimamia ubora wa bidhaa,ikiwepo shirika la viwango nchini (TBS) ili kuhakikisha nguzo zinazonunuliwa zinakidhi viwango vinavyotakiwa na shirika hilo.
Makamba alisema kuwa ili kuondoa changamoto kwa wadau wa nguzo na serikali ataunda kamati y wadau wa nguzo watakaokuwa wanafuatilia namna ya utengenezaji wa nguzo bora za umeme ambao utasaidia kuuza nje ya nchi ambavyo wadau wanguzo nchi nyingine wanafanya kwa ubora unaotakiwa.
“Sasa ipo mifano ya mfumo huu wa uwekezaji wa viwanda vya nguzo,nchi kama Afrika Kusini inamfumo mzuri sana na serikali yenu ipo tayari kuwachukua watu kadhaa kwenye kila wadau na kuwapeleka na kuwalipia mkajifunze kuhusu mfumo wa kudhibiti na kuhusu ubora” alisema makamba
Aidha aliwatoa hofu wadau wa
nguzo za Miti za Umeme nchini kwa kuwahakikishia soko la kuuza nguzo zenye
ubora kwa Shirika la Umeme nchini( TANESCO) na Wakala wa Nishati Vijijini (
REA), hapa nchini.
Makamba alisema kuwa mkutano ulilenga kuondoa sintofahamu pamoja na minong’ono
inayoendelea kwa baadhi ya watu wanaopotosha kuwa Serikali haitanunua nguzo za
Umeme za ndani na badala yake zitaagizwa kutoka nje ya Nchi.
Katika mazungumzo yake na Wadau hao, Makamba alisema kuwa, Serikali itaendelea
kununua nguzo za miti za Umeme kutoka kwa wazalishaji wa ndani ili kulinda
viwanda vya ndani kwa kuzingatia ubora wa nguzo uliowekwa.
“Tutakapo toa zabuni ili ufanikiwe kupata zabuni hiyo lazima angalau asilimia Fulani ya nguzo hizo utakazouza ziwe zimetoka ka watu wadogo wadogo na katika nyaraka yako ya kuomba zabuni iwepo ili ufanikiwa angalau asilimia 20 au 10 ya nguzo iwe inatoka kwa wadau wadogo na wawe wamepewa mikataba inayoeleweka” alisema Makamba
Makamba amewataka Wadau hao kuunda chama Cha wazalishaji wa nguzo ili kiweze kudhibiti ubora unaotakiwa na hata kutoa adhabu kali kwa atakayebainika kuzalisha chini ya Kiwango pamoja na kuandaa sheria zitakazoongoza chama hicho.
“Lengo la Serikali ni kukuza uchumi wa wananchi wake kwa kuboresha bidhaa zao
kwa kuwasimamia katika kuzalisha kwa vigezo na ubora uliowekwa, ili wananchi
hao waweze kunufaika na kukuza uchumi wao na pato la Taifa kwa ujumla” Alisema
Makamba.
Kwa Upande wake Mkurugenzi
Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO), Maharagwe Change, aliwataka
Wadau hao kuwa waaminifu pale nguzo zao zinapotakiwa kupelekwa katika maeneo ya
miradi kwa kuweka nguzo halisi zilizokaguliwa na siyo kufanya udanganyifu wa
kuweka zisizokuwa na ubora.
Amesema kumekuwa na changamoto ya nguzo kuharibika baada ya muda mfupi kutumika
kutokana na kuwa chini ya kiwango na ubora unaotakiwa, huku nguzo hizo zikiwa
tayari zimekaguliwa na kuonekana zina ubora unaotakiwa.
Naye Mkurugenzi Mkuu wa Wakala
wa Nishati Vijijini (REA), Mhandisi Hassan Said, amewahakikishia Wadau hao kuwa
soko la nguzo lipo la kutosha kwani bado miradi mingi ya usambazaji wa Umeme
vijijini inaendelea na nguzo nyingi zinahitajika.
Akitoa mfano Mkoa wa Iringa kuwa kuna Mradi wa Ujazilizi ambao unatarajia
kuanza hivi karibuni katika Mkoa huo na mikoa mingine.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Queen Sendiga amewapongeza wabunge wa Mkoa wa Iringa Kwa kuwa wamoja Katika kutetea ajenda za kimaendeleo zinazohusu Mkoa wa Iringa.
Alisema kuwa umoja ambao wameonesha kwenye kupigania suala la nguzo za Umeme kuendelea kununuliwa hapa hapa Nchini wamefanya Jambo la kizalendo sana kwani linaenda kuongeza mapato kwa serikali na Wananchi kwa ujumla. Vivyo hivyo amewataka kuendelea kufanya hivyo kwenye ajenda nyingine za ki mkoa .
Sendiga Alisema kuwa Mkoa wa Iringa na Njombe ndio ambao wameuza nguzo zaidi ya asilimia 90 zilizotumika kusambaza Umeme nchini na walishangazwa kusikia hoja ya kuwa nguzo za ndani sio bora wakati tayari nguzo nyingi zimesimikwa Vijijini na zipo imara
"Tukushukuru Mheshimiwa Waziri wa Nishati kwa kufanya maamuzi haya ambayo yana Afya kubwa Kwa uchumi wa mikoa hii miwili na Taifa"
Amewataka Wadau hao kutoa ushirikiano kwa mamlaka husika na kuwa wasikivu kwa kile watakachokuwa wakielezwa kwa lengo la kupata bidhaa Bora kwa manufaa yao na taifa kwa jumla.
Sendiga alisema kuwa baada ya suala la nguzo kumalizika wabunge hao wana wajibu wa kuendelea kusukuma ajenda ya Mkoa wa Iringa ya ujenzi wa barabara ya kiwango cha Lami toka Iringa hadi Ruaha Kwa ajili ya kuchochea kasi ya utalii ndani ya hifadhi ya Taifa ya Ruaha
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.