Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kwamba ingawa Tanzania imeondolewa kwenye nchi zenye uchumi wa kati lakini kufikia mwaka 2025 Tanzania itakuwa imefika au imekaribia kurudi uchumi wa kati.
Mhe. Rais Samia ameyasema hayo leo Aprili 5, 2022 alipokuwa akihutubia katika hafla ya kufungua mkutano wa kitaifa wa haki, amani na maridhiano Tanzania ambao umefanyika Makao Makuu, Dodoma.
"Tanzania tuliingia uchumi wa kati tukarudishwa, siyo kwa mipango ya mtu, ni mipango ya Mungu. Kwahiyo tupambane kurudi tulipokuwa. Na kwa ninavyoiongoza serikali, natarajia kufikia 2025 tutakuwa tumefika au tunakaribia kurudi uchumi wa kati" - Rais Samia Suluhu Hassan.
Aidha katika hotuba yake, Rais Samia amewasisitiza viongozi wa vyama vya kisiasa kuhakikisha kwamba wanautumia mkutano huo vema na kumpelekea mapendekezo yenye tija kwa Tanzania na watu wake.
Rais Samia amewakumbusha wajumbe wa mkutano huo kuwa Tanzania itajengwa na watanzania wenyewe na hivyo wajadili mambo ambayo yanaendana na mazingira ya Kitanzania na kuongeza kwamba kazi ya vyama vingi ni kuona yanayofanywa na serikali na kutoa maoni kwa serikali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.