WITO umetolewa kwa viongozi wa Mashirika, Taasisi na Idara zote zilizo na wafanyakazi walioajiriwa kutoa ruksa za ibada kwa wafanyakazi wao waliokwenye mfungo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhani ili watumishi hao wazidi kuthamini ajira walizo nazo na kuzitumikia kwa ufanisi.
Hayo yamesemwa na Sheikh wa Mkoa wa Mwanza Hassan Kabeke mara baada ya kushiriki iftar iliyoandaliwa na Benki ya KBC Tawi la Mwanza na kuwafuturisha wateja wake wa Kanda ya Ziwa, huku benki hiyo ikitumia mwanya huo kutambulisha huduma yake ya mikopo isiyo na riba yaani SAHL BANK. "Unaonaje wewe bosi, wewe kiongozi kwenye taasisi au shirika flani ukawa na mfanyakazi mwenye kumweshimu na kumwogopa Mungu?, Bila shaka mfanyakazi huyo atakuwa msaada mkubwa kwako" amesema Sheikh KabekeTupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.