ZAHARA Shaaban (31), ambaye ni mjamzito, ameshukuru namna alivyookolewa na msamaria mwema kutoka kwenye basi lililopata ajali kwa kupitishwa dirishani .
Mama huyo ni miongoni mwa majeruhi 26, waliolazwa katika hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Morogoro, baada ya kutokea kwa ajali ya basi la Ahmeed Coach, lilokuwa likitokea mkoani Mbeya kwenda jijini Tanga na kusababisha vifo 23.
Zahara amezungumza na kusema yeye ni mzaliwa wa Tanga, lakini ameolewa mkoani Iringa na alikuwa anasafiri na basi hilo kwenda nyumbani kwao, eneo la Mwanzange au kwa jina lingine Mwakazalu, Tanga kusubiri muda wa kujifungua.
“ Kutokana na hali yangu hii ya kuelekea kujifungua, nilionelea bora niende kwetu nyumbani Tanga, kujisubiria kujifungua, “ amesema Zahara.
Anasema alipata siti ya kukaa kwenye basi hilo, lakini alisema kuna mua alikuwa amechoka, hivyo kuamua kulala chini kwenye ‘korido’ ya basi hilo.
“ Wakati hii ajali inatokea sikuweza kujua au kuona kilichotendeka zaidi ya kushituka baada ya kutokea kishindo, kikubwa na kuangukiwa na mizigo iliyowekwa pembezoni ndani ya basi hili,” amesema.
Mizigo hiyo ilimwangukia kwenye mguu wa kulia na kifuani pamoja na abiria aliyekua kwenye siti ya karibu yake alipokuwa amelala chini, ambaye alimlalia juu.
“ Mtu mmoja amenisaidia kwanza kumtoa aliyenilalia, kunichomoa na kunitoa kupitia kwenye dirisha na nikapokelewa nje ya dirisha na mfugaji wa Kimasai, wakanilaza chini kwenye majani nipate hewa na nikaingizwa kwenye gari hadi hospitalini
“ Nawashukuru madaktari na waauguzi, nimevunjika mguu wa kulia kwenye kifundo …nilipata maumivu ya kifuani na michubuko midogo mguu wa kushoto,” amesema Zahara.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Fortunatus Musilim ameeleza ajali hiyo ilitokea jana Machi 18, saa 10 alasiri na chanzo ni dereva wa Lori lenya namba za IT 2816 likitokea Dar es Salaam kwenda nchi jirani ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), lililokuwa linamkwepa mwendesha pikipiki, hivyo kugongana uso kwa uso na basi ya Ahmeed lenye namba T 732 ATH .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.