ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 23, 2021

WAZIRI MKUU WA UFARANSA AKUTWA NA VIRUSI VYA CORONA.

 


Waziri Mkuu wa Ufaransa Jean Castex amekutwa na virusi vya Corona, saa chache tu baada ya kurejea kutoka ziara ya nchi jirani ya Ubelgiji. 

Taarifa ya Waziri Mkuu huyo kukutwa na virusi vya Corona imetolewa katika wakati ambapo Ufaransa inashuhudia ongezeko la maambukizo ya ugonjwa wa Covid-19. 

Baada ya tangazo hilo, Waziri Mkuu wa Ubelgiji Alexander De Croo na mawaziri wengine wanne wamelazimika kukaa karantini baada ya kukutana na Castex kwa mazungumzo mjini Brussels mapema Jumatatu. 

Ofisi ya Waziri Mkuu huyo wa Ufaransa imesema atalazimika kuendelea na shughuli zake za kikazi akiwa karantini kwa siku 10 zijazo. Licha ya kuwa asilimia 75 ya wakaazi wa Ufaransa kuchomwa chanjo, idadi ya wagonjwa wa Covid-19 imeongezeka katika wiki za hivi karibuni. 

Rais Emmanuel Macron alikutwa na virusi vya Corona Disemba mwaka uliopita, wakati mawaziri wengine wa serikali yake pia wamewahi kuambukizwa virusi hivyo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.