Taasisi ya kudhibiti magonjwa nchini Ujerumani ya Robert Koch imeweka wazi takwimu mpya za maambukizo ya virusi vya corona nchini ikisema idadi imeongezeka zaidi katika kipindi cha siku saba.
Kwa mujibu wa taasisi hiyo, takwimu mpya zinaonesha visa vipya 45,326 vimeongezeka katika kipindi cha siku moja ikiwa ni ongezeko kubwa ikilinganishwa na wiki iliyopita ambapo kulikuwa na maambukizo mapya 32,048 yaliyoropitiwa.
Data zilizotolewa leo Jumanne zinaonesha watu 309 wamekufa kutokana na Covid-19 nchi nzima ndani ya kipindi cha saa 24, idadi hiyo ikiwa imeongezeka kutoka 265 iliyoripotiwa wiki iliyopita.
Takwimu mpya zinaonesha kwa ujumla watu milioni 5,430,911 wameambukizwa nchini Ujerumani ingawa maafisa wanaamini idadi inaweza kuwa kubwa zaidi kwa sababu visa vingi havitambuliwi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.