ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 23, 2021

MADEREVA 537 WAFUTIWA LESENI.

 


Madereva 537 wamefutiwa leseni za kuendesha magari kuanzia mwezi JanuarI hadi Septemba mwaka huu kutokana na kukiuka sheria za usalama barabara.

Mkuu wa Kikosi cha usalama barabarani, Willbroad Mtafungwa ametoa taarifa hiyo leo Jumanne Novemba 23, 2021 katika uzinduzi wa wiki ya usalama barabara kitaifa ambayo inafanyika jijini Arusha.

Mtafungwa amesema madereva hao wamefungiwa leseni kutokana na kukithiri kwa matukio yao ya kuvunja sheria.

Amesema madereva 472 katika kipindi hicho wamefikishwa mahakamani kutokana na makosa hayo ya usalama barabarani.

Hata hivyo amesema matukio ya makosa ya usalama barabarani yamekuwa yakipungua kila mwaka kuanzia mwaka 2018 hadi mwaka 2021.

Amesema bado ajali nyingi zinasababishwa na mwendokasi wa madereva, ulevi, kutovaa mikanda, kutokuwa na vidhibiti vya kuwalinda watoto, kutovaa kufika nguvu na kupita magari bila tahadhari.

Ameiomba Serikali kusaidia baraza la usalama barabarani fedha za ununuzi vifaa vya kisasa vya ukaguzi magari, kusaidiwa kupata fedha kununua kamera za barabarani za CCTV ili kudhibiti ajali lakini pia kuwa na ruzuku maalum Kwa baraza hilo.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.