ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 17, 2021

BARCELONA INA DENI LA £1.15 BILLION: RAIS WA BARCELONA.

 



Rais wa klabu ya Barcelona Joan Laporta amefichua kwamba klabu hiyo ya Uhispania ina deni la £1.15bn, akiitaja hali hiyo kuwa ya wasiwasi sana.

Deni la kulipa mishahara ya klabu hiyo kwa sasa ni asilimia 103 ya jumla ya pato lote la klabu.

Laporta amemlaumu mtangulizi wake Josep Maria Bartomeu kwa deni hilo, akimshutumu kwa kuiwacha klabu hiyo katika hali mbaya.

‘’Iwapo tungemuongezea kandarasi Lionel Messi, deni la mishahara lingefikia asilimia 110 ya pato lote, suala ambalo ligi ya La Liga ilikataa kukubali’’.

Messi alitangaza kuondoka katika klabu hiyo katika hotuba iliojawa na hisia wiki iliopita na kuingia katika kandarasi ya miaka miwili na klabu ya PSG.

‘’Mishahara yetu inawakilisha asilimia 103 ya pato la jumla la klabu hii , hiyo ni sawa na kati ya asilimia 20-25 zaidi ya washindani wetu’’, alisema Laporta, akiwa katika kipindi cha pili cha uongozi wake tangu aliposhinda uchaguzi wa mwezi Machi.

‘’Kitu cha kwanza tulichofanya tulipowasili tulilazimika kuomba mkopo wa Yuro milioni 80 , la sivyo tungeshindwa kulipa mishahara. Utawala uliopita ulikuwa na udanganyifu chungu nzima’’.

‘’Barcelona ina upungufu wa Yuro milioni 451 – ni urithi mbaya sana . Kile ambacho kimekuwa kikifanyika kinatia wasiwasi’’.

Bartomeu alijitetea katika barua ya wazisiku ya Jumamosi , akidai kwamba mikakati ya kifedha ambayo angeweka iwapo asingelazimishwa kujiuzulumwezi Oktoba ingemruhusu Messi kusalia Barcelona.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.