ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, March 10, 2020

UKEREWE WAZINDUA ZOEZI LA KUNYUNYIZIA DAWA YA UKUKO KUPAMBANA NA TISHIO LA MALARIA


Katika tafiti za viashiria vya ugonjwa wa malaria zilizofanyika hivi karibuni mwaka 2017, Mkoa wetu wa Mwanza bado umeonekana kuwa na kiwango kikubwa cha maabukizi ya ugonjwa wa malaria kwa asilimia 8.1. Kiwango hiki kiko juu ya kiwango cha Taifa ambacho ni asilimia 7.3. Aidha matokeo ya upimaji wa vimelea vya malaria kwa watoto wa Shule za Msingi uliofanyika mwaka 2017 na 2019,Wilaya ya Ukerewe ilionekana kuwa na kiwango kikubwa cha watoto wenye vimelea vya malaria kwa asilimia 51 mwaka 2017 na asilimia 44.2 mwaka 2019. Takwimu za Afya zinazotokana na mfumo wa Wizara ya Afya, katika kipindi cha miaka mitatu mfurulizo Wilaya ya Ukerewe imeonekana kuwa na kiwango kikubwa cha wagonjwa waliothibitika kuwa na vimelea vya ugonjwa wa malaria, yaani asilimia 52.6 ya wagonjwa waliotumwa maabara kupima malaria mwaka 2017 walikutwa na vimelea vya malari, asilimia 51.4 kwa mwaka 2018 na asilimia 51.1 kwa mwaka 2019. Kwa hali hiyo ya ukubwa wa tatizo la ugonjwa huo katika Wilaya ya Ukerewe, serikali imeamua kupambana kuongeza afua za kudhibiti malaria katika Wilaya hiyo ambapo safari hii Mkuu wa Mkoa wa Mwanza John Mongella mguu kwa mguu anafanya ziara ya kazi wilayani humo na kushiriki uzinduzi wa zoezi la uangamizaji wa viluviluvi wa Mbu waenezao Malaria kwa kutumia viuadudu vya dawa maarufu ya UKOKO.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.