Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wachimbaji Wadogo Nchini, John Bina amewasilisha ombi kwa Balozi wa Tanzania nchini China Mbelwa Kairuki, akimwomba balozi kuzungumza na wawekezaji toka taifa hilo kuona jinsi gani wanaweza kusaidia wachimbaji nchini katika uwezeshaji wa vifaa na vitendea kazi vya uchimbaji wa madini, teknolojia na suala la mitaji.
Akizungumza katika MKUTANO WA FURSA ZA UWEKEZAJI WA TEKNOLOJIA MITAJI NA MASOKO YA MADINI NCHINI UNAOFANYIKA ROCK CITY MWANZA na kuhudhuriwa na wachimbaji wadogo na viongozi wa sekta hiyo toka mikoa yote nchini, Bina amesema kutokana na shirikisho lake kuwa na rasilimali watu ya kutosha anaimani ushirikiano ukijengwa kati yao na Ubalozi wanauwezo wa kukopesheka kwa kupatiwa mkopo wa vifaa na nyenzo za kisasa za uchimbaji ili wanachama wake waweze kukodisha na kupitia kipato kitakachopatikana kulipa deni la mkopo.
Aidha Rais huyo amewasihi wachimbaji hao kutojihusisha na suala la utoroshaji madini, akisema serikali tayari imekwisha weka mfumo rafiki kwao kufanya biashara bila hofu ya kukimbilia njia za panya kuhofia tozo zisizoeleweka.
Pia Rais huyo wa Shirikisho ameiomba Serikali kutoa ufafanuzi juu ya taratibu za kuuza bidhaa nje ya nchi na zuio lake kwa kufafanua ni madini gani yanaruhusiwa kusafirishwa na madini gani hasiyoruhusiwa.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.