ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, November 11, 2019

WENGI HUOFIA KUANDIKA WOSIA KWA KUOGOPA KUFANYIZIWA


WOSIA ni maansishi maalum yaliyoandikwa na mtu kabla hajafariki ambayo yanakuwa na ujumbe kuhusu mtu fulani au mali baada ya kufariki.

moja ya mambo ambayo yamesahaulika kwa jamii ambayo hayapewi kipaumbela ni miongoni mwa hili la wosia ambapo husababisha migogoro katika familia nyingi nchini.

Licha ya Serikali kuhamasisha wananchi kuandika wosia ili kuepusha migogoro katika familia mwitikio umekuwa mdogo kwa watu wa mijini na vijijini, kitendo ambacho husababisha mjane, watoto wa marehemu kupoteza mali zao kwa kunyang'anywa na ndugu au jamaa.

Wapo baadhi ya ndugu ambao wanatabia ya kutolea macho vitu vilivyoachwa na marehemu pindi anapofariki kwa sababu hajaacha wosia wowote na kusababisha migogoro katika familia hasa siku ya matanga.

Pi wapo baadhi ya watu wanashindwa kumhudumia ndugu yao ambaye ana mali nyingi na badala yake wanakuwa wanamwombea kufariki ili waweze kujitwalia mali zake huku familia yake hususani wajane na watoto wakibaki wakiishi mazingira ya shida wakati hawakustahili kuishi hivyo.

Kwa kuyaona yote haya na mengine mengi shirika lisilo la kiserikali linalojihusisha na utetezi wa haki za wanawake na watoto (KIVULINI) limekuja na programu ya kutoa elimu sanjari na kugawa maandiko yaliyo andikwa mfumo rahisi wa wosia.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.