ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, November 12, 2019

AJALI MBAYA YA TRENI YAUWA WATU TAKRIBAN 16 NCHINI BANGLADESH

Watu takriban 16 wameripotiwa kupoteza maisha baada  ya treni mbili kugongana mashariki mwa Bangladesh.

Kulingana na ripoti ya vyombo vya habari Bangladesh, ajali hiyo imetokea katika mkoa wa Brahmanbaria, kilomita 100 mashariki mwa mji mkuu Dhaka baada ya treni mbili kugongana majira ya asubuhi.

Timu za uokoaji zimethibitisha kuwa watu takriban 16 wamepoteza maisha huku angalau wengine 40 wakiwa wamejeruhiwa.

Kuna uwezekano kuwa idadi ya waliopoteza maisha kuongezeka kutokana na hali mbaya ya baadhi ya majeruhi.

Sababu kuu iliyosababisha ajali hiyo mbaya ya treni kugongana haijajulikana bado.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.