ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Wednesday, November 20, 2019

RAIS MAGUFULI KUFANYA ZIARA YA KWANZA DODOMA.



Mkuu wa Mkoa wa Dodoma, Dk.Binilith Mahenge (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu ziara ya Rais Dk. John Magufuli ambayo inataraji kuanza kesho Novemba 21 hadi 25 mkoani humo. Kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Dodoma, Patrobas Katambi.

Miongoni mwa shughuli atakazofanya ni kesho kuwa mgeni rasmi katika Mahafali ya 10 ya Chuo Kikuu cha Dodoma.

Ijumaa atatembelea na kuweka jiwe l msingi kwemye mradi wa Hospitali ya Uhuru Wilayani Chamwino, ujenzi wa Nyumba za Askari 118, Ujenzi wa Stendi Kuu ya mabasi na Soko Kuu la Dodoma zilizopo Nzuguni nankuzungumza na wananchi.

Jumatatu Novemba 25, Rais ataweka mawe ya msingi kwemye ujenzi wa miradi ya Makao Makuu ya JWTZ Kikombo, Ujenzinwa Ofisi za Uhamiaji na Jengo la Makandarasi.

Hii itakua ni ziara ya kwanza tangu ahamia rasmi Dodoma tangu atangaze kuhamia Oktoba 12,2019.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.