TAREHE 17 october 2019 katika kituo cha afya Buzuruga uzinduzi wa kimkoa wa kampeni shirikishi ya chanjo ya surua-rubella, umefanyika ukishuhudiwa na Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia, Wazee na Watoto Dr. Zainabu Chaula aliyeambatana na mwenyeji wake Mkuu wa Mkoa huo John Mongella.
Zoezi la chanjo hufanyika kila baada ya miaka mitatu tokea kampeni iliyopita. Kampeni ya mwisho ilifanyika nchini mwaka 2014 ambapo ufanisi katika mkoa wa Mwanza ulikuwa ni asilimia 97.
Katika Kampeni ya mwaka huu zitatolewa chanjo za Surua na Rubella pamoja na chanjo ya Polio. walengwa wa chanjo Chanjo ya Surua na Rubella ni watoto wote wenye umri kati ya miezi 9 hadi miaka mitano kamili.
Kwa Chanjo ya Polio walengwa ni watoto wote wenye umri kati ya mwaka mmoja na nusu na miaka mitatu na nusu.
Mkoa wa Mwanza unataraji kuchanja jumla ya watoto 637,579 dhidi ya Surua-Rubella na watoto 266,140 dhidi ya ugonjwa wa Polio. Chanjo hizi ni salama zimethibitishwa ba Shirika la Afya Ulimwenguni na DSerikali ya Tanzania kupitia Mamlaka ya Dawa Tanzania.
Mkoa wa Mwanza una Jumla ya Vituo 608 vya kutolea chanjo hizi. Vituo hivi viko kwenye vituo vya huduma za Afya ama shule ama eneo lolote lililo karibu na makazi ya wananchi.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.