ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Friday, October 18, 2019

DAR ES SALAAM YAONGOZA TENA KWA WALIOJIANDIKISHA UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA.Na Ezekiel Mtonyole, Dodoma.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, TAMISEMI, Selemani Jafo amewapongeza viongozi na wananchi wa Mkoa wa Dar es saalam kwa kuitikia kikamilifu zoezi la uandikishaji katika orodha ya wapiga kura na kuongoza kwa zoezi hilo katika orodha ya mkoa.

Waziri Jafo ameyasema hayo leo Jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari kuhusu hali ya uandikishaji katika daftari la orodha ya wapiga kura mara baada ya kufikia hitimisho siku ya Jana Octoba 17.

Amesema Mkoa wa Dar es saalam mwanzo ulianza kwa kusuasua lakini  baada ya kuanza kupeana hamasa wameweza kufanya vizuri, amesema viongozi wa kazi zote na wananchi kwa ujumla hatimaye kufanikiwa kwa kuandikisha kwa asilimia 108.

"Niwapongeze Mkoa wa Dar es saalam wakati natangaza kwa mara ya kwanza Mkoa ulikuwa na hali mbaya lakini viongozi wa ngazi zote wamehamasishana halikadhalika wananchi kwa kiwango kikubwa hadi kuongoza niwapongeze sana" amesema Waziri Jafo.

Aidha amesema kwa mujibu wa Ofisi ya Takwimu wananchi wenye sifa ya kupiga kura ni 26,960,485, lakini walijiwekea lengo la kuandikisha wapiga kura milioni 22,916,412 ambao ni sawa na asilimia 85, ya wananchi wenye sifa ya kupiga kura (wanaume 10,924,479) na wanawake 11,991,933.

Amesema baadhi ya maeneo yalikumbwa na changamoto mbalimbali ikiwamo mvua na baadhi ya vituo kuwa mbali na makazi ya watu, hivyo baada ya siku ya mwisho waliamua kuongeza siku tatu kwa ajili ya kuhakikisha kila mtu anapata fulsa ya kujiandikisha.

Ameongeza kuwa "hadi kufikia Octoba 17 jumla ya wapiga kura 19,681,259 walikuwa wamejiandikisha katika orodha ya daftari la wapiga kura kwa mwaka 2019, Kati ya hao wanaume 9,529,992 na wanawake10,151,267, sawa na asilimia 86, ya lengo la wapiga kura 22,916,412, na huu ndio uandikishaji wenye mafanikio zaidi ukilinganisha na mwaka 2014" amesema.

Licha ya kila Mkoa kuvuka lengo lakuandikisha kwa asilimia 50,  Mkoa mitano iliyoongoza ni Dar es saalam 108%, Pwani 96%, Mwanza 95%, Tanga 90% na Singida 90% na wote wamezawadiwa kikombe maalamu.

Huku Mikoa mitano ya mwisho licha ya kuvuka lengo lakini imeshika nafasi tano za mwisho, wa mwisho kabisa ni Kigoma 65%, Njombe 75%, Simiyu na Shinyanga 76%, ambayo jumla ya Mkoa yote ni 86%.

"Kwa upande wa halmashauri zilizofanya vizuri ni Mlele 152%, Ngorongoro 129%, Kibiti 126%, Temeke 122% na Monduli 122% ,na halmashauri zenye wapigakura wengi zaidi ya laki tisa 90,000 iliyoongoza ni Temeke MC 122%, Ilala MC111%, Mwanza CC 105%, Ubungo MC 103% na Kinondoni MC 96%" amesema.

Aidha amewapongeza wananchi wote waliojitokeza, na viongozi wa ngazi zote kuanzia mikoa na vitongoji kwa kuhamasisha katika kujiandikisha kwenye daftari la orodha ya wapiga kura la uchaguzi wa serikali za mitaa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.