Afisa elimu sekondari wilaya ya Mufindi Musa Ally akiongea na wanafunzi wakati wa ziara ya Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa shuleni hapo
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiongea na wanafunzi wa shule ya sekondari Ifwagi alipofanya ziara ya kikazi katika shule hiyo
Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa akiwa sambamba na afisa elimu sekondari wilaya ya Mufindi Musa Ally na mtendaji wa kata ya Ifwagi wakati wa ziara ya mbunge huyo katika shule hiyo
NA FREDY MGUNDA,IRINGA.
Wanafunzi wa shule ya sekondari
ya Ifwagi iliyopo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa wametakiwa kufaulu kwa
kiwango cha kupata daraja la kwanza ili waweze kupata fursa ya kupata ufadhili
wa kusomeshwa na Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa.
Akizungumza wakati
alipotembelea shuleni hapo Mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini Mahmoud Mgimwa
alisema kuwa mwanafunzi atakayepata daraja la kwanza atamsomesha kwa kumlipia
baadhi ya mahitaji muhimu kuanzia kidato cha tano hadi chuo kikuu.
“Mimi nipo tayari kuchangia
baadhi ya mahitaji kwa wanafunzi watakao faulu vizuri katika mtihani wa mwisho
wa kidato cha nne ambapo mnatarajia hivi karibuni mtafanya mtihani huo”alisema
Mgimwa
Mgimwa alisema kufanya hivyo
kutaongeza chachu ya wananfunzi kusoma kwa bidii na kuwa na ufaulu ambao
utaleta maendeleo ya mwanafunzi na shule yenyewe hivyo mnatakiwa kusoma kwa
bidii na kuzingatia masomo yenu ili mpate matokeo mazuri ya mtihani wa mwisho.
Aidha Mgimwa alisema kuwa
anaendelea kuboresha sekta ya elimu kwa kujenda mabweni katika shule mbalimbali
za jimbo la Mufindi Kaskazini hivyo hata hapa Ifwagi tunaendelea na ujenzi wa
bweni kwa lengo la kuhakikisha tunaboresha elimu na kukuza ufaulu kwa wanafunzi
wa shule hii.
“Nimechangia fedha nyingi
kwenye bweni lenu hili ambalo ndio kwanza tumeanza hivyo mtuombee kwa mungu ili
tukamilishe ndoto ya ujenzi wa bweni hili na wanafunzi mnatakiwa kudhamini
mchangao wa wazazi,walimu,mbunge wenu na serikali kwa ujumla kwa juhudi ambazo
zinafanywa kuleta maendeleo” alisema Mgimwa”
Mgimwa aliongeza kwa kusema
kuwa katika shule ya sekondari ya Ifwagi amechangia katika ujenzi wa vyoo,bweni,uchimbaji
wa kisima pamoja na kushughulikia maswala ya michezo hivyo rai yake kwa
wanafunzi ni kuhakikisha wanasoma kwa bidii ili yapatikane matokeo mazuri.
Naye afisa elimu sekondari wilaya ya Mufindi Musa
Ally alimpongeza mbunge wa jimbo la Mufindi Kaskazini kwa juhudi anazozifanya
kuhakikisha anaboresha sekta ya elimu kwa kuchangia kila mara kwenye shule zote
zilizopo katika jimbo hilo.
“Huyu mbunge amekuwa msaada
sana kwetu maana kila mara tukiomba msaada wowote unahusu elimu amekuwa
akitusaidia kwa hali na mali ni tofauti na wabunge wengine hivyo mnapaswa hata
kuwaambia wazazi wenu mchango wa mbunge huyu kwenye sekta ya elimu” alisema
Ally
Kwa upande wao baadhi ya
wanafunzi wa shule hiyo ya sekondari ya Ifwagi walimpogeza mbunge huyo na
kumuomba aendelee kuwasaidia kuboresha elimu kwa kuwa elimu ndi msingi mkuu wa
maisha ya mwanadamu
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.