ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Tuesday, August 6, 2019

YALIYOJIRI WAKATI WA UFUNGUZI WA MAONESHO YA NNE YA WIKI YA VIWANDA YA JUMUIYA YA MAENDELEO YA NCHI ZA KUSINI MWA AFRIKA (SADC) LEO TAREHE 5 AGOSTI, 2019 #Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Magufuli

# Viwanda ni muhimu katika kukuza uchumi, kuondoa umaskini na kuongeza ajira, viwanda ndivyo vimeziletea maendeleo makubwa nchi zilizoendelea.

# Nazipongeza nchi za SADC kwa Kuchukua hatua za kukuza sekta ya viwanda na ikiwa mkakati huu utatekelezwa utasaidia kukuza uchumi wa nchi zetu hizi

# Historia ya mataifa yaliyoendelea yanatufundisha ni lazima kupitia katika mapinduzi ya viwanda.

# Mchango wa Sekta ya viwanda katika nchi za Afrika na SADC bado ni mdogo sana, sekta hii inachangia wastani wa asilimia 10 ya pato la taifa na katika jumuiya ya SADC inachangia asilimia 11 pekee.

#Sisi wanachama wa SADC tujikite katika kukuza na kuendelela ubunifu kwa watu wetu na kuendeleza teknolojia rahisi ya viwanda, tuwaendeleze vijana wetu, tuendeleze viwanda vidogo vidogo

# Ukosefu wa viwanda unaifanya Afrika iendelee kuwa na uchumi tegemezi na hivyo kubaki katika mduara wa umaskini hii ndio gharama ya kutokuwa na viwanda.

#Wiki ya viwanda ya SADC ni fursa ya kubadilishana uzoefu miongoni mwa wadau kuhusu utekelezaji wa mikakati ya miaka 49 ya uendelezaji wa viwanda katika jumuiya yetu.

# Kauli mbiu ya wiki ya viwanda ni muafaka kwa mwaka huu ambapo mataifa yetu yanapambana kuondoa vikwazo mbalimbali vya uwekezaji hususani katika viwanda na kuhamasisha ushiriki mpana wa sekta binafsi.

#Bado tuna safari ndefu ya kuhakikisha sekta ya viwanda inazidi kukua na kuleta mageuzi ya kiuchumi katika nchi zetu

# Tuweke kipaumbele kwenye uhuishwaji wa teknolojia ya viwanda ndani ya jumuiya yetu na ndani ya Afrika.

# Tuuziane malighafi na bidhaa nyingine miongoni mwetu ili tukuze mitaji na kuendeleza viwanda ndani ya jumuiya na bara letu kwa ujumla.

# Tujikite kwenye kukuza na kuendeleza ubunifu wa watu wetu pamoja na kuhamasisha matumizi ya teknolojia rahisi.  #Tushugulike vikwazo vinavyochelewesha maendeleo ya sekta ya viwanda ndani ya SADC na ndani ya Afrika.

#Ndani ya nchi za SADC kuna fursa nyingi za uwekezaji wa Viwanda ikiwemo Madini, kilimo, Uvuvi,

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.