WAKATI ulimwengu ukiadhimisha wiki ya kimataifa ya kunyonyesha mtoto (Agosti 1 hadi 7) na kuelezea faida zake kwa wazazi na taifa, wakazi wa jiji la Mwanza, kwenye kata mbalimbali na viunga vyake tofauti tofauti wanaendelea kuhamasishwa kufahamu umuhimu wa maziwa ya mwanzo kabisa ya mama kwa mtoto .
Shirika la Amref Health Africa kwa kushirikiana na Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto, Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania (TFNC) na Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) linatekeleza programu ya Lishe kupitia programu ya 'Right Start Initiative' inayolenga kuboresha huduma za lishe kwa wakinamama wajawazito, watoto wachanga na watoto chini ya miaka miwili na wasichana wa rika balehe katika mikoa ya Mwanza na Simiyu.
SHUHUDIA YALIYOJIRI SIKU YA PILI YA UELIMISHAJI KATA YA MHANDU WILAYANI NYAMAGANA MKOANI MWANZA. (CHUNGULIA VIDEO)
* DONDOO ZA AFYA NA KUNYONYESHA
Kunyonyesha ni moja ya njia sahihi ya kuhakikisha mtoto anakuwa mwenye afya na kuendelea kuishi.
Kama viwango vya kunyonyesha vingekuwa vya hali ya juu duniani , takriban maisha 820 000 ya watoto yangenusurika kila mwaka, linasema shirika la afya duniani (WHO).
Unyonyeshaji wa mtoto kwa miezi 6 kuna faida nyingi za kiafya kwa mama na mtoto.
Kumnyonyesha mtoto mara anapozaliwa kwa kipindi cha saa moja, humkinga kwa maambukizi yanayowapata watoto wachanga na kupunguza vifo vya watoto wachanga.
Maziwa ya mama pia ni chanzo muhimu cha nguvu na virutubisho kwa watoto wa kati ya miezi 6 hadi 23.
Maziwa ya mama yanaweza kuchangia nusu au zaidi ya nguvu za mtoto katika umri wa miaka 6 hadi 12.
Watoto na vijana wadogo walionyonyeshwa wakiwa wachanga wana uwezekano mdogo wa kuwa na uzito wa mwili wa kupindukia .
Unyonyeshaji wa mtoto humsaidia kuboresha uwezo wa utambuzi wa akili (IQ), mahudhurio ya shule , na pia huhusishwa na mapato ya juu katika maisha yake ya utu uzima.
Kunyonyeshwa kwa muda mrefu pia huchangia afya na maisha bora ya mama kwani humpunguzia hatari ya kupata saratani ya mfuko wa mayai ya uzazi na matiti.
Kunyonyesha hutengeneza vichocheo vyamwili( hormone) ambazo humtuliza mama na mtoto.
Juma hili linaadhimishwa huku baadhi ya wanawake duniani wakishindwa kuwanyonyesha watoto wao ipasavyo kutokana na sababu mbali mbali. .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.