Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Dk. Bashiru Ally amehudhuria Mkutano Mkuu wa Jimbo la Ilemela wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani ya CCM Jimbo la Ilemela-uwanja wa CCM Kirumba.
Mkutano huo maalum wa uwasilishaji wa utekelezaji wa Ilani, uliofanywa na Mbunge wa Ilemela, Angelina Mabula umehudhuriwa viongozi mbalimbali wa chama na serikali wakiongozwa Wajumbe wa Kamati Kuu ya CCM Ndg. Kheri James Mwenyekiti wa Vijana wa CCM taifa na Mama Munde Tambwe, mjumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa ndg. Jamal Babu, viongozi wa Mkoa, Wilaya, Kata, Matawi na wajumbe wote wa mashina Wilaya ya Ilemela.
Katibu Mkuu akizungumza katika mkutano huo, ametoa maelekezo kwa viongozi wa serikali hasa wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya kusimamia vipimo vya ujazo wa mazao ikiwemo kupiga marufuku ujazaji wa rumbesa na mizani isiyotenda haki kwa wakulima.
"Natoa maelekezo nchi nzima kwa wakuu wa mikoa na wilaya kwa niaba ya CCM, kama mnataka kazi ndani ya serikali hii ya CCM nisisikie malalamiko kuhusu ujazaji wa rumbesa kama ambavyo baadhi ya wafanyabiashara wanawafanyia wakulima wetu hivi sasa. Rumbesa, na mizani isiyokuwa ya haki kwa wakulima wetu ni kosa kisheria, na kamati za siasa za mikoa, wilaya, kata na matawi simamieni hili na mtoe taarifa ili wananchi wanyonge wasiendelee kunyanyaswa." Dk. Bashiru ameelekeza.
"Ninawaomba vijana nchi nzima, tuendelee kuwalinda viongozi wa chama na serikali dhidi ya yeyote anayetoa kejeli kwa kazi kubwa wanazofanya viongozi wetu usiku na mchana, hatutaruhusu mwenyekiti na Rais wetu, Katibu Mkuu wetu na viongozi wote wakatishwe tamaa na watu wachache wasioitakia mema nchi yetu." Ndg. Kheri amesisitiza.
Mkuu wa mkoa wa Mwanza John Mongella akitoa neno la utambulisho na makaribisho kwa wadau waliohudhuria mkutano huo.
Ziara hii ya siku tano, imeanza leo Mkoani Mwanza ikiwa ni muendelezo wa kutekeleza jukumu la viongozi wa CCM kufuatilia utekelezaji wa maelekezo ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.