Askari kutoka kikosi cha mbwa na Farasi wakifuatilia mada.
Afisa Mawasiliano Mwandamizi wa TBL Group, Amanda Walter, (wa tatu Kulia) akimkabidhi Kaimu Kamanda wa Polisi Kikosi cha Mbwa na Farasi Tanzania, ASP Kyariga, msaada wa vifaa vya kusaidia ukarabati wa ofisi baada ya kufanya ziara kiwandani hapo na kupatiwa mafunzo ya Unywaji wa Kistaarabu.
--- Kampuni ya Tanzania Breweries Limited (TBL) chini ya kampuni ya kimataifa ya ABInBev, mwishoni mwa wiki imeendesha semina ya unywaji kistaarabu kwa askari polisi kutoka kituo Mbwa na Farasi, jijini Dar es Salaam, ikiwa ni mwendelezo wake wa kufikisha elimu hiyo katika makundi mbalimbali ya kijamii.
Akiongea baada ya semina hiyo,Meneja Mawasiliano wa TBL, Amanda Walter, alisema kuwa kampuni hiyo imekuwa ikiendesha kampeni zake nyingi zilizolenga kufikia jamii kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi na inaamini Jeshi hilo linalo fursa kubwa kufanya kazi na jamii kupitia mtandao wake ulioenea nchini kote.
"Jeshi la Polisi ni wadau wetu wakubwa katika kampeni mbalimbali ikiwemo za kuelimisha jamii masuala ya Usalama na ndio maana tunaamini kupitia kwao kampeni ya kuhamasisha unywaji wa pombe kistaarabu itawafikia wananchi nchi wengi na ndio maana tunawapatia elimu hii na tutaendelea siku zote kufanya kazi kwa karibu na taasisi mbalimbali za Serikali na zisizo za Serikali ajenda yetu ya kujenga ‘Dunia maridhawa", alisema Walter.
TBL kwa muda wa miaka mingi imekuwa ikiunga mkono jitihada za Serikali za kupunguza matukio ya ajali nchini, hususani za barabarani kwa kushirikiana na Kikosi cha Polisi cha Usalama Barabarani na wadau wengine kutoa elimu ya Unywaji wa pombe kistaarabu.
Mwishoni mwa mwaka jana, kwa kushirikiana na Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, SUMATRA, TANROADS na kampuni ya usafirishaji abiria ya UBER, ilizundua kampeni kubwa iliyopata mafanikio makubwa kwa kuwafikia watanzania wengi ya ‘Kamata Usukani wa Maisha Yako’ ambayo iliwalenga madereva wanaoendesha vyombo vya moto kwa kuwakumbuka kuwa unywaji wa pombe na kuendesha vyombo vya moto hakuendani.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.