Kwa vyovyote vile, Barcelona chini ya kocha Ernesto Valverde watakuwa na kila sababu ya kujiamini pale watakapominyana na Manchester United kesho Jumatano katika mchezo wa raundi ya kwanza ya robo fainali ya Klabu Bingwa Ulaya katika dimba wa Old Trafford.
Licha ya kuwa na mafanikio mazuri nyumbani, kwa sasa Klabu Bingwa Ulaya ndiyo kipaumbele namba moja kwa klabu hiyo na mashabiki wake kote ulimwenguni.
Miamba hiyo imekuwa ikiyaaga mashindano hayo katika hatua ya robo fainali kwa miaka mitatu mfululizo iliyopita.
Katika kipindi chote hicho, habari mbaya zaid kwa Barcelona ilikuwa ni, mahasimu wao wa jadi, klabu ya Real Madrid ndiyo ilikuwa ikinyanyua ndoo.
Tayari Messi ameshawaahidi mashabiki wa Barcelona mwanzoni mwa msimu huu kuwa: "Tunaahidi kuwa tutafanya kila tuliwezalo ili kulirudisha kombe lile zuri hapa Camp Nou."
Lakini Manchester United hawatakiwi kukata tamaa kabisa, sababu Barcelona wanafungika.
Udhaifu mkubwa wa Barcelona ni safu yake ya ulinzi, ambayo kwa mara kadhaa imedhihirisha kuwa haiwezi kuzuia mashambulizi ya kushtukiza. Hilo lilionekana wazi kwenye sare yao ya 4-4 na Villarreal ambao wanambana ili kujinusuru na kushuka daraja.
Barca pia kwa miaka ya hivi karibuni hawana rekodi safi katika mechi za ugenini katika hatua ya mtoano kwenye kombe la Klabu Bingwa.
Barca hawajashinda mechi yoyote kwenye hatua ya mtoano toka walipoifunga Arsenal 2-0 Februari 2016 - na kwenye kipindi hicho wamepokea vipigo vizito ugenini kutoka kwa Atletico (2-0), Paris St Germain (4-0), Juventus (3-0) na Roma (3-0).
Hivyo, kuna kila sababu kwa United kuamini kuwa wanaweza kuiadhibu Barcelona inayoongozwa kikamilifu na Lionel Messi, lakini haitakuwa kazi rahisi.
WEWE UNAMAONI GANI?
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.