SERIKALI imezindua kitaifa mafunzo kwa wafugaji yenye lengo la kuzijua Sheria za Mifugo na kutambua haki zao ili kujiepusha na migogoro baina yao na majirani zao wakiwemo wakulima, wahifadhi pamoja na kuelimishwa mbinu za kisasa za namna ya kuboresha maisha na ufugaji .
Akizindua mafunzo hayo kitaifa katika Kijiji cha Kimotorok wilayani Simanjiro mkoani Manyara, Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Luhaga Mpina amesema mafunzo hayo yatawawezesha wafugaji kutambua namna ya kutumia fedha zitokanazo na mifugo na mazao yake kwa kuwekeza maeneo mengine, kujenga makazi bora, kusomesha watoto, kukata bima ya mifugo na kujiwekea akiba benki .
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.