Hatma ya ombi la mbunge wa Arumeru Mashariki JoshuaNassari juu ya kufungua kesi ya msingi ya kutengua uamuzi wa Spika wa Bunge wa kumvua ubunge inatarajiwa kuamuliwa Machi 29 mwaka huu.
Shauri hilo linasikilizwa katika mahakama kuu ya Dodoma na Jaji Latifa Mansur huku upande wa serikali ukiwakilishwa na mawakili watatu na upande wa mlalamikaji ukiwa na wawili ambapo uamuzi huo utatolewa baada ya Jaji Latifa kusikiliza mapingamizi matatu yaliyowasilishwa na serikali kutokana na ombi la Nassari.
Wakati shauri la mbunge huyo la kufungua kesi likisikilizwa imeibua ubishani kati ya pande mbili zilizovutana kutokana na kanuni ya kudumu ya bunge kifungu namba 146(3) iliyomvua ubunge mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki (CHADEMA) Joshua Nassari kwa takribani masaa manne.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.