ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Saturday, December 1, 2018

ZEE LATIA MIMBA MWANAFUNZI 'LAKIONA CHA MTEMA KUNI'



GSENGOtV

Katika siku ya 4 mara baada ya mafunzo kwa vitendo  ya jinsi ya kumkwamua mtoto wa kike toka kwenye wingu la ukatili na mbinu ya jinsi ya kuvidhibiti, viongozi wa kada mbalimbali washiriki wanatinga katika mtaa wa KanyaMwanza kata ya Mwabaluhi wilayani Sengerema, na kulianzisha tena.

IGIZO
Zee la miaka yake latongoza binti wa shule hata kumpatia mimba, laswekwa gerezani na adhabu kali, nini jamii inasema kuhusu mikasa kama hiyo?

 Fuatilia kuona nini sababu.

Mpango wa kuielimisha jamii kwa kutumia maigizo kupitia watu maarufu na wanaotambulika katika nyadhifa mbalimbali kwenye jamii na ngazi mbalimbali serikalini, umekuja kama mbinu mpya kukabiliana na yale yanayochangia vitendo vya ukatili dhidi ya watoto hususani mtoto wa kike.

Badala ya kutumia vikundi vya sanaa, Wakuu wa wilaya, Wakurugenzi, Mabwana na Mabibi afya, Wachungaji, Mashekhe, Viongozi jumuiya ya wazazi, Makatibu Tawala, Wenyeviti na Makatibu Watendaji wa vijiji na vitongoji ndiyo wamekuwa wasanii.

Ni katika mradi wa mwaka mzima uliochini ya FAWE Tanzania, ukiratibiwa na Shirika la Elimu, Sayansi na Utamaduni la Umoja wa Mataifa (UNESCO) na kufadhiliwa na Shirika la Maendeleo la Korea (KOICA)

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.