GSENGOtv
Mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella ameagiza vyombo vya dola mkoani hapa kuchukua hatua dhidi watu waliohusika kuvujisha mtihani wa darasa la saba na kusababisha serikali kuingia gharama ya kurudiwa kwa mtihani huo.
Akizungumza jijini hapa, Mongella ameagiza jeshi la Polisi na taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa –TAKUKURU, mkoani Mwanza kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wakuu wa shule za Alliance, New Alliance na Kisiwani za jijini hapa na wote wanaotuhumiwa kuhusika na udanganyifu wa mitihani ya kitaifa ya darasa la saba 2018.
Akionesha kukerwa na kitendo hicho alichokiita cha aibu na fedheha kwa mustakbar wa elimu ya Tanzania, Mongella amesema serikali itachukua hatua kali dhidi ya wale wote waliohusika kuvujisha mitihani hiyo bila ya kumuonea mtu yeyote.
Kufuatia tukio hilo serikali imetoa nafasi kwa wanafunzi wa shule hizo kurudia mitihani hiyo tarehe 8 na tarehe 9 mwezi huu katika vituo vitakavyotangazwa na serikali.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.