Akizungumza kwa niaba ya Mbunge Jimbo la Nyamagana Mhe. Stanslaus Mabula, Mwenyekiti wa taasis ya First Community Organizations Ndg. Ahmed Misanga ametoa salamu za Mbunge ambaye yupo safarini nchini Ujerumani Kikazi, amewapongeza wahitimu kwa kuhitimu kidato cha nne.
Na kuwaasa kutumia elimu hiyo kuisadia jamii na kujiendeleza kimasomo hadi kufikia daraja la stashahada, shada, shahada ya Uzamili hadi shahada ya Uvamivu. Mhe. Mabula amenituma niwaambie anawatakia maandalizi mema ya mitihani kufuzu kidato cha nne wanafunzi wote wa wilaya yetu ya Nyamagana pamoja na Tanzania nzima mnamo tarehe 5 Ndg Misanga amesema.
Wahitimu wakisoma Risala kwa mgeni rasmi mbali kwa kuainisha mafanikio waliyoyapata ikiwa ni pamoja na maadili mema, stadi za kazi na elimu ya darasani kwa uwiano wa Mwalimu 1 wanafunzi 20 kadharika wamewasilisha ombi la kusaidia kutatuliwa changamoto ya ukosefu wa Bwaro la Chakula pamoja na jengo la Makitaba.
Mahafari haya ya tisa yalipambwa na maonesho maalum ya kazi za wanafunzi, upandaji wa miti. Yalihudhuliwa na Katibu wa Mbunge Jimbo la Nyamagana, mkuu wa shule Sosthenes Malegesi Mgunda, Mkurugenzi wa shule Isaacs Manyonyi, pamoja na wageni mbali mbali waalikwa Mwalimu chuo kikuu cha Arusha Paul Semba, Afisa elimu wilaya na kata, Mtendaji kata pamoja na Mwenyekiti wa serikali ya mtaa wa Mahina kati.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.