ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

ZIMA KILA KITU ILA WASHA JEMBE FM 93.7 MWANZA

Monday, October 15, 2018

HIVI NDIVYO MWANZA ILIVYO MUENZI HAYATI BABA WA TAIFA


GSENGOtV

TAREHE 14 October 2018, Tanzania imeadhimisha kumbukumbu ya miaka 19 bila uwepo wa Baba wa Taifa Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Licha ya maeneo mbalimbali nchini kujumuika sehemu kadhaa kwaajili ya ibada na kuadhimisha kumbukumbu hiyo, mkoa wa Mwanza nao haukuwa nyuma, Chama cha Mapinduzi Mkoa kimefanya kusanyiko lake la maadhimisho katika viwanja vya Mchafukoga kata ya Igogo wilayani Nyamagana.

Shughuli mbalimbali za kumuenzi Baba wa Taifa zimefanyika ikiwa ni pamoja na Maandamano ya amani, Ngoma za asili, Mchezo alioupenda wa Bao, Chipukizi kuonesha ufundi wao katika gwaride na mapigo ya karate vilevile wazee wamepata nafasi ya kueleza  jinsi walivyomfahamu Mwalimu.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. John Mongella ndiye aliyekuwa mgeni rasmi wa maadhimisho hayo kimkoa naye anasema kukamilika kwa adhma ya Serikali kuwapa bure huduma bora za afya wazee wetu ndiyo njia stahili kumuenzi Hayati Baba wa Taifa.

Tupe maoni yako

0 comments:

Post a Comment

Note: Only a member of this blog may post a comment.