Jeshi la polisi mkoani Arusha, linawasaka watu kadhaa wanaotuhumiwa kuharibu gari la mbunge wa viti maalum mkoa wa Manyara, CHADEMA, Anna Gidarya kwa kuchoma matairi kwa kutumia kitu chenye ncha kali.
Jeshi la Polisi mkoani humo, limeeleza kuwa tukio hilo lilitokea jana Septemba 16, 2018, majira ya saa 1:00 Asubuhi, barabara kuu ya Arusha – Karatu katika kitongoji cha Majengo kata ya Mto wa Mbu tarafa ya Manyara wilayani Monduli na limeshatolewa taarifa katika kituo cha Polisi Mto wa Mbu.
Tukio hilo lilitokea barabarani wakati Mbunge akiwa na wenzake watatu kwenye gari, wakakutana na watu wengine waliokuwa kwenye gari jingine, ambapo walizozana na kisha mtu mmoja alishuka na kuchoma kwa kitu nyenye ncha kali Magurudumu ya gari alilokuwa amepanda Mbunge na kisha kutoweka.
Akiongea na www.eatv.tv mchana huu kamanda Ng'anzi amesema tayari wameshazipata namba za gari ambalo walikuwemo watu hao hivyo kinachoendelea sasa ni kuwatafuta kwa kutumia namba hizo.
''Bado tunaendelea na zoezi la kuwatafuta watu hao, na tayari tumeshapata namba za gari waliyokuwa wamepanda kwahiyo tutawakamata tu kwa kutumia namba hizo'', ameeleza.
Tupe maoni yako
0 comments:
Post a Comment
Note: Only a member of this blog may post a comment.